CURRENT NEWS

Wednesday, December 20, 2017

DKT. NDUGULILE ASHIRIKI UJENZI WA SHULE KATIKA ZOEZI LA KUAMSHA ARI YA WANANCHI KUFANYA SHUGHULI ZA MAENDELEO WILAYANI KISARAWE.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt Faustine Ndugulile akishiriki kuchanganya mchanga wa kutengeneza  zege kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Msingi Chambasiwakati wa zoezi la kuamsha ari ya wananchi katika kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao katika wilaya ya Kisarawe.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt Faustine Ndugulile akishiriki kutengeneza tofali wakati wa zoezi la kuamsha ari ya wananchi katika kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao aliposhiriki katika ujenzi wa shule ya Msingi Chambasi wilayani Kisarawe.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt Faustine Ndugulile akishiriki kubeba ndoo ya zege wakati wa zoezi la kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao aliposhiriki katika ujenzi wa shule ya Msingi Chambasi wilayani Kisarawe.

Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Bibi.Sihaba Nkinga akishiriki kubeba ndoo ya zege wakati wa zoezi la kuamsha ari ya wananchi katika kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao aliposhiriki katika ujenzi wa shule ya Msingi Chambasi wilayani Kisarawe.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt Faustine Ndugulile akizungumza na wananchi wa kijiji cha  wakati wa zoezi la kuamsha ari ya wananchi hao kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao aliposhiriki katika ujenzi wa shule ya Msingi Chambasi wilayani Kisarawe.Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt Faustine Ndugulile akifurahi pamoja na wananchi wa kijiji chaChambasi mara baada ya kushiriki ujenzi wa  shule ya msingi Chambasi wakati wa zoezi la kuamsha ari ya wananchi katika kufanya shughuli za maendeleo katika maeneo yao wilayani Kisarawe.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

   ..................................................................................................................................... 
Na Kitengo cha Mawailiano WAMJW

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt Faustine Ndugulile ameshiriki kazi ya ujenzi wa shule ya msingi Chambasi Wilayani Kisarawe ikiwa ni zoezi la kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Dk. Ndugulile amesema kuwa kwa kipindi kirefu dhana ya wananchi kujitolea katika kufanya kazi za maendeleo imepungua kwa kiasi kikubwa na kuiachia Serikali ikitoa kila kitu kutekeleza miradi ya maendeleo hata kama inawezekana kazi hizo kutekelezwa na wananchi.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa kwa kipindi cha sasa cha Serikali ya Awamu ya Tano ya Hapa kazi tu wananchi hawana budi kujitoa katika kufanya shughuli za maendeleo katika maeneno hayo ili kuisaidia Serikali na kujisaidia wao wenyewe kujiletea maendeleo.

“Msisubiri kila kitu kifanywe na Serikali vingine mnaweza kufanya weneyewe hongereni sana ninyi ni mfano wa kuigwa kwa vijiji vingine katika hili” alisema Dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Chambasi Bi. Fodia Makebu Tungaraza amesema kuwa mradi huo wa ujenzi wa shule umeibuliwa na wananchi wenyewe mara baada ya watoto wao kutembea umbali mrefu kwenda kijiji cha jirani kuifata shule ya Msingi Msimbu takribani kilomita sita hivyo kuhatarisha maisha na usalama wa wanafunzi hao.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msimbu Bw. Hussein Mkambara ambae pia anayesimamia shule ya Chambasi hadi itakapopata usajili ameishukuru Serikali kwa kuona na kuwaunga mkono katika jiitihada za kujikwamua katika changamoto waliyokuwa nayo kwa kipindi kirefu.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt Faustine Ndugulile amefanya ziara ya siku moja mkoani Pwani wilaya ya Kisarawe kwa kushiriki ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Chambasi, kuvitembelea vikundi vya wanawake vinavyojishughulisha na biashara na viwanda vidogo vidogo vinaowezeshwa na Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake na kutembelea Mahakama inayohusika na mashauri ya watoto wilayani Kisarawe.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania