CURRENT NEWS

Saturday, December 9, 2017

FAMILIA YA MWANAMZIKI NGUZA VIKING MAARUFU KAMA BABU SEYA SASA IPO HURU


Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta JOHN MAGUFULI, leo amewaongoza Watanzania katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara, huku akitangaza kuwasamehe Wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa Kunyongwa.
          Aidha, Rais MAGUFULI ametangaza kuachiwa Huru Familia ya Mwanamziki Nguza Viki maarufu kama Babu Seya waliofungwa Maisha katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam, kutokana na kosa la Kunajisi Watoto.
          Mbali na msamaha huo ambao ametumia Ibara ya 45 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais MAGUFULI, ametangaza kuwapunguzia adhabu Wafungwa 8,157, ambapo kati yao zaidi ya Elfu-2 wataachiwa leo na wengine Elfu Sita waliobaki watatoka baadaye.
          Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Rais MAGUFULI, amesema sio kwamba wote waliofungwa Kunyongwa walitenda makosa hayo, huku pia akisisitiza kuwa kati ya Wafungwa hao wapo wenye umri wa miaka 85.
          Katika kutekeleza agizo lake, amemkabidhi Waziri Mkuu, KASSIM MAJALIWA orodha ya Wafungwa 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa akitaka ashugulikie ili waondolewe Gerezani.
          Idadi hiyo ya msamaha kwa Wafungwa inatajwa kuwa ni kubwa katika awamu zote kuwahi kutokea na hasa zinazo wahusisha Wafungwa wa Kunyongwa na Vifungo vya Maisha.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania