Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa
na viongozi wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora wakielekea kwenye kukagua jengo
jipya la upasuaji katika Kituo cha Afya cha Zogolo.
Viongozi wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora wakipata
maelekezo ya matumizi ya Tiles kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tamisemi Selemani Jafo.
.........................................................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewaagiza
wahandisi wa ujenzi katika Halmashauri zote hapa nchini kuona uwezekano wa
kutumia Tiles badala ya kuweka sakafu ya kawaida ili kuongeza uimara na mandhari
majengo hayo.
Waziri Jafo ametoa maelekezo hayo alipokuwa akikagua ujenzi wa
madarasa na mabweni ya shule ya sekondari Hamza na miundombinu mbalimbali
ya kituo cha afya cha zogolo yakiwepo majengo ya upasuaji, maabara, na wodi
ambapo majengo yote ameyakuta yamejengwa vizuri sana kwa kuwekwa Tiles.
Ameeleza kwamba majengo mengi yanayojengwa na kuwekwa floor(sakafu)
ya kawaida yanabomoka kwa muda mfupi na hivyo kuhitajika kufanyiwa ukarabati
mara kwa mara.
Waziri Jafo amesisitiza kwamba ujenzi wa kutumia Tiles kusaidia
hata katika usafi wa majengo hayo.
Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amewapongeza viongozi wa wilaya
ya Nzega wakiwemo wabunge wao Hussein Bashe, Selemani Zedi, na Hamisi Kigwangwala
kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwahudumia wananchi wao.
Post a Comment