CURRENT NEWS

Friday, December 22, 2017

JAFO AKERWA NA UCHAFU SOKO LA MABIBO.

      
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani jafo akifanya ukaguzi katika soko la mabibo.


 Waziri w Nchi,Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani jafo akiwa na Meya wa Ubungo akijionea madimbwi na tope kwenye soko la mabibo.


Wafanyabiashara wa soko la mabibo wakitoa malalamiko yao kwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani  Jafo.
       ............................................................................

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo ameonyeshwa kukerwa na uchafu uliokithiri katika soko la Mabibo lililopo wilayani Ubungo jijini  Dar as salaam. 

Soko hilo maarufu kwa jina la Mabibo-mahakama ya ndizi limetapakaa maji machafu na madibwi yanayotoa harufu mbaya.   

Jafo amesema uchafu huo ni hatari sana kwa afya ya wananchi kwani wanaweza kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa kipindupindu.

Kutokana na hali hiyo, Jafo ameielekeza manispaa ya ubungo kufanya marekebisho ya haraka ikiwa ni pamoja na kufukia madimbwi na kusambaza kokoto sokoni hapo pamoja na kuweka mfereji wa kupitishia maji.

Pia Jafo amewataka watendaji wa soko hilo kusimamia mapato ipasavyo kutokana na ukusanyaji mapato kuwa hauridhishi.

Amesema  wastani wa sh.milioni 90 kwa mwezi zinakusanywa ikilinganishwa na biashara kubwa ya ndizi na viazi inayofanywa sokoni hapo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania