CURRENT NEWS

Sunday, December 24, 2017

JAFO APONGEZA KAMATI YA UJENZI WA MIRADI ZA VIJIJI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa ameambatana na viongozi wa wilaya ya Kisarawe katika ukaguzi wa mradi wa maji Kwala-Chole.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wa wilaya ya Kisarawe wakikagua ujenzi unaoendelea wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Mitengwe.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akikagua nyumba ya daktari ambayo ipo kwenye hatua za mwisho za ujenzi katika kituo cha Afya Maneromango.

Baadhi ya miondombinu iliyojengwa kwenye Kituo cha Afya Maneromango.

    ........................................................................................

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo amezipongeza kamati zinazosimamia ujenzi wa miradi kwa kutumia utaratibu wa ‘Force Account’ hapa nchini kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo yenye ubora na inayozingatia thamani ya fedha. 

Jafo alitoa pongezi hizo alipokuwa akikagua miradi ya maendeleo wilayani Kisarawe ambapo alifanikiwa kukagua ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule za msingi Mitengwe, Kitonga Mango, Boga, mapoja na kituo cha Afya Maneromango.

Amesema ujenzi huo umetumia utaratibu huo wa ‘Force Account’ ambapo miundombinu mbalimbali imejengwa kwa gharama nafuu pamoja na kutoa ajira kwa mafundi wanaopatikana katika maeneo miradi hiyo inapotekelezwa.

Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa pia kukagua jengo jipya la upasuaji, maabara, wodi ya kinamama, nyumba ya daktari, jengo la kuhifadhi maiti, vyumba 12 vya madarasa mapya, matundu ya vyoo 30, pamoja na Ofisi za walimu 3.

Mbali na hilo, Waziri Jafo amekagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa maji Kwala-Chole ambao unagharimu zaidi ya sh. billion 1.8 na ameagiza mradi huo ukamilike ifikapo mwishoni mwa mwezi Machi 2018.

Amewataka wananchi kote nchini kushiriki kulinda na kusimamia rasilimali fedha zinazopelekwa katika vijiji vyao kwaajili ya maendeleo.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania