CURRENT NEWS

Saturday, December 16, 2017

JAFO ASEMA HATAMVUMILIA YEYOTE ATAKAYEHUSIKA NA RUSHWA TARURA.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akifunga mafunzo ya manunuzi kwa maafisa wa Tarura.


Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya maafisa Tarura.
           ......................................................

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, TAMISEMI  Selemani Jafo amewaonya watumishi wa Wakala wa barabara Mijini na Vijijini(TARURA) mikoani na wilayani kutojihusisha na masuala ya Rushwa wakati wanatimiza majukumu yao kwa kuwa watakaojihusisha watachukuliwa hatua kali zikiwemo kutimuliwa kazini.

 Jafo aliyasema hayo alipokuwa anafunga mafunzo hayo jijini mwanza kwa maafisa wa TARURA wa wilaya na mikoa kutoka mikoa ya kanda ya ziwa ikihusishwa Mwanza, Mara, Shinyanga, simiyu, Geita, kagera, Kigoma, na Tabora.

Katika mafunzo hayo,washiriki wa mafunzo hayo wamejengewa uwezo katika swala la manunuzi, mikataba, maadili, Rushwa, Jinsia, Ukimwi, pamoja na afya na usalama mahala pa kazi.

 Mafunzo kama haya yamesha kamilika katika kanda zingine za kaskazini, na kanda  mashariki na Kati na yanatarajiwa kukamilishwa kwa mikoa iliyobaki ya kanda za juu kusini mwanzoni mwa mwezi Januari 2018.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania