CURRENT NEWS

Thursday, December 14, 2017

JAFO ASHTUKIA MAKUSANYO YA HOSPITALI MISUNGWI

    
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi.

  
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua hospitali ya wilaya ya Misungwi.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akipata taarifa ya miradi ya elimu kutoka kwa viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua ujenzi wa maabara katika sekondari ya Misasi.

         ...................................................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo ametilia shaka makusanyo katika hospitali ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na kuagiza kusimamiwa vyema ukusanyaji mapato.

Jafo ameyasema hayo katika ziara yake ya kikazi ndani ya Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo alisema amegundua kuna kila dalili kwamba mapato ya hospitali hiyo yanavuja kutokana na taarifa nyingi za fedha za Malipo ya wagonjwa kutoingizwa kwenye mfumo wa kielekroniki hivyo kusababisha kukusanya wastani wa Sh.milioni 4 kwa mwezi. 

Katika ziara hiyo, Jafo amezungumza na watumishi wa Halmashauri ya Misungwi ambapo amewasisitiza watumishi na viongozi kuwa na mahusiano mema ili waweze kuwaletea maendeleo wananchi wa wilaya hiyo.

Jafo amesisitiza kwamba kila mmoja anapasa kumthamini mwenzake na kushirikiana katika kazi ili kuwaletea wananchi maendeleo.


Aidha Jafo amewapongeza walimu wa shule ya sekondari Misasi kwa kufanya vyema sana kwani wamefanikiwa kupeleka watoto 45 kidato cha tano kati ya wanafunzi 100 waliomaliza kudato cha nne mwaka jana.


Baada ya ziara hiyo waziri Jafo ameendelea na ziara yake wilayani sengerema mkoani Mwanza
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania