CURRENT NEWS

Sunday, December 17, 2017

JAFO AWATIA MATUMBO JOTO WATAALAM WA KILIMO NCHINI


 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akitoa maagizo baada ya kukagua mashamba na kubaini hayajapandwa kwa utaratibu wilayani Nzega.

 Baadhi ya mashamba aliyokaguliwa na kukutwa yamepandwa kiholela wilayani Nzega.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa katika ukaguzi wa utekelezaji wa maagizo yake kwa wataalam wa kilimo  katika vijiji vya wilaya ya Nzega.

    ...........................................................................................

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo ameanza kuwapima wataalam wa kilimo kivitendo hapa nchini baada ya maelekezo yake aliyo yatoa miezi miwili iliyopita kwa wataalam wote wa kilimo hapa nchini kuwafikia wakulima kwa kuwapa elimu ya kilimo badala ya kukaa ofisini.

Lengo la agizo hilo ni  kuongeza uzalishaji kwa kufuata kanuni za kilimo bora.

Akiwa wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Jafo amepata nafasi kutembelea mashamba ya wakulima na kubaini hawajapata ushauri wowote wa kitaalam.

“Inawezekana wataalam wengi wa kilimo wamechukulia poa agizo leo nimeanza ukaguzi mashamba nimefika hapa nimekuta mashamba yamepandwa hovyo hovyo bila kufuata kanuni za kilimo bora,”amesema

Kutokana na hali hiyo, Waziri Jafo aliwajia juu maafisa kilimo na kuwaonya kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Waziri Jafo ametoa onyo kwa afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya  Nzega na kumtaka ajirekebishe kabla hajachukuliwa hatua kali za kiutumishi.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania