CURRENT NEWS

Tuesday, December 26, 2017

KIONGOZI CCM MKOANI SINGIDA APATA AJALI AKIWA NA FAMILIA YAKE

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Juma Kilimba, mkewe na watoto wao watatu wamejeruhiwa baada ya gari kupinduka eneo la Msigiri wilayani Iramba.


Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Jamson Mhagama akizungumza na MCL Digital amesema ajali imetokea leo Jumatatu Desemba 25,2017 mchana na hali zao zinaendelea vizuri.

Mhagama amesema Kilimba amelazwa katika Hospitali ya Kiomboi.

Amesema mkewe Kilimba na wanawe wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Itigi.

Mhagama amesema CCM mkoani Singida inaendelea kusimamia matibabu yao.

Amesema mmoja kati ya watoto hao anapata huduma katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU).
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania