CURRENT NEWS

Friday, December 15, 2017

MAVUNDE AWATAKA VIJANA WASOMI KUUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI KATIKA KUPAMBANA NA RUSHWA.Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde amewataka vijana wasomi wa nchi kuwa mstari wa mbele kuunga mkono kazi nzuri na kubwa anayofanya Rais John Magufuli katika kupambana na Rushwa, Ufisadi na Udhalimu.

Mavunde ameyasema hayo jana katika ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre-Dar es salaam wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya Viongozi wa Vyuo vikuu nchini juu ya masuala ya Maadili ya viongozi na rushwa.

Amehimiza Vijana wasomi kutambua nafasi yao katika Jamii na kutambua kwamba Taifa hili linawategemea kwa ustawi wake hivyo lazima wawe mstari wa mbele kuhakikisha kwamba tunajenga Taifa la Vijana wenye maadili lakini pia Vijana ambao watakuwa mstari wa mbele katika kupambana na Rushwa na aina yoyote ya udhalimu.


Aidha,Mwenyekiti wa Tahliso Stanslaus Peter Kaduguze amewashukuru Taasisi ya Uongozi kwa kufanikisha mafunzo hayo ambayo anaamini yamebadilisha fikra na mtizamo wa Vijana wengi wasomi juu ya masuala ya Maadili na Vita dhidi ya rushwa.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania