CURRENT NEWS

Friday, December 22, 2017

MAVUNDE KUENDESHA OPARESHENI MAALUM YA KUKAGUA WAAJIRI AMBAO HAWAJATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MHAGAMA LA KUJIUNGA NA MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI(WCF) NCHINI


 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akizindua miongozo ya utekelezaji wa majukumu ya Baraza la Wafanyakazi mfuko wa fidia kwa Wafanyakazi(WCF).

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akiteta jambo na  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha mshomba.

 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akionyesha miongozo ya utekelezaji majukumu ya baraza la wafanyakazi wa WCF kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha mshomba.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akizungumza kwenye kikao cha baraza la wafanyakazi wa WCF.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde akizungumza na waandishi wa habari.

         ........................................................................

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde ameendelea kukazia maagizo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mh Jenister Mhagama aliyoyatoa kuwataka waajiri wote wawe wamejisajili katika mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF) kwa kubainisha kwamba kwasasa inaendelea operesheni maalum ya kuhakikisha maagizo hayo ya waajiri kujisajili katika mfuko wa fidia yanatekelezwa kwa mujibu wa sheria.

Mavunde ameyasema hayo leo wakati akifungua Baraza la kwanza la Wafanyakazi wa mfuko wa fidia kwa Wafanyakazi(WCF)katika makao makuu ya ofisi za WCF Jijini Dar es salaam.

Amesema waajiri wote nchini wanapaswa kutekeleza sharti la kisheria la kujiunga na mfuko wa huo wa fidia ili kuilinda nguvu kazi ya Tanzania kutokana na madhara/magonjwa yatokanayo na kazi na kuahidi kwamba atalisimamia agizo la Waziri Mhagama kwa kuendesha operesheni ya ukaguzi nchi nzima kubaini waajiri ambao bado hawajatekeleza takwa hilo la kisheria.

Naibu Waziri Mavunde amesema watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa WCF Masha Mshomba amebainisha kwamba Mwajiri yoyote atakayekutwa  hajajisajili katika Mfuko atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwamo faini isiyozidi Tsh.milioni  50 au kifungo cha miaka 5 Jela kwa Mkuu wa Taasisi husika au vyote kwa pamoja kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi No. 20 ya Mwaka 2008..
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania