CURRENT NEWS

Friday, December 22, 2017

MEYA KINONDONI SITTA AKABIDHI HUNDI ZA MILIONI 200 KWA KATA 20 ZA MANISPAA YA KINONDONI KILA KATA MILIONI 10 ZA VIKUNDI VYA WAKINA WANAWAKE NA VIJANA LEO
Katika Kutekeleza Matokeo Chanya kwa Maendeleo ya Taifa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 kwa Kumuunga Mkono kwa Vitendo Rais Dkt.John Magufuli Manispaa ya Kinondoni wameamua Kutenga Fedha asilimia 10 ya Mapato yatokanayo na Manispaa ya Kinondoni ambayo kwa Mwaka wa fedha 2017/2018 ilikuwa ni BILIONI 2 Kwa leo kwa awamu ya Kwanza Vimekabidhiwa Milioni 200 kwa Vikundi vilivyokidhi vigezo 
Mh.Meya Sitta amewataka Vijana Kuchangamkia Fursa ya Mikopo hiyo ndani ya Manispaa kwani Wanawake ndiyo wamejitokeza kwa wingi kuliko vijana.
Pia amewataka Vijana wakinondoni Kuacha kulalamika Sasa Mwisho waende Katika Ofisi za Maafisa Maendeleo Jamii katika Kata zao Kufuata utaratibu wa Namna ya Usajili vikundi pia waweze kunufaika na mikopo hiyo ,Fedha zilizobaki ni Bilioni Moja na Milioni Mia nane kwa Mwaka wa Fedha  2017/18.

Imetolewa na Mwandishi
James Mwakibinga.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania