
Milingoti ya bendera za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwa bila bendera ikiwa ni kuomboleza mauaji ya askari wa Tanzania waliouawa wakilinda amani chini ya Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. (Picha:UN/Idhaa ya Kiswahili/Leah Mushi)
Miili ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa 14 waliouawa katika mashambulizi huko kivu ya kaskazini, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongpo-DRC mwishoni mwa wiki iliyopita imewasili nchini kwa ajili ya mipango ya mazishi.
Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York nchini Marekani, bendera za nchi wanachama 193 hazijapandishwa katika milingoti na ya Umoja wa Mataifa ikipepea nusu mlingoti.
Hii ni ishara ya maombolezo ya walinda amani hao kutoka Tanzania waliouawa na wengine 53 kujeruhiwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Miili ya walinda amani wa Tanzania waliouawa wakati wa mapigano huko Semuliki, jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Hapa ni Beni wakati wa kuaga miili hiyo ambayo tayari wamewasili Dar es salaam. (Picha:MONUSCO)
Tayari Umoja wa Mataifa likiwemo Baraza la usalama la wamelaani vikali mauaji hayo na kusema kuwa yanafifisha juhudi za kutafuta suluhu katika jamuhuri ya kidemokrasia Kongo DRC.
Post a Comment