Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
akikagua ujeniz wa barabara ya lami inayojengwa na Wakala wa Barabara Mijini na
Vijijini(Tarura) mjini Sengerema.
Tenki la kuchuja maji mradi wa Buyagu
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Sengerema
..................................................................................
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tamisemi Selemani Jafo
amemuagiza mkandarasi wa mradi wa maji Buyagu kukamilisha mradi huo kabla
mwishoni mwa mwezi Februari 2018 la sivyo ataingia matatani.
Jafo alionyesha kukerwa kutokana na utendaji duni ulionyeshwa na
mkandarasi huyo D4N Co. Ltd.
Mradi huo ulianza mwaka 2014 na unagharimu shilingi za
kitanzania bilioni 1.7
Katika ziara hiyo wilayani sengerema Jafo amewasihi watendaji
kujituma wakati wanatimiza majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.
Waziri Jafo alifanikiwa kutembelea mradi mwingine wa ujenzi wa
barabara ya lami na amemuagiza meneja wa Tarura Halmashauri ya Sengerema
kusimamia ubora wa barabara zinazojengwa katika Halmashauri hiyo.
Post a Comment