CURRENT NEWS

Sunday, December 31, 2017

MKUU WA WILAYA YA CHEMBA AFANYA ZIARA YA SIKU MOJA KATIKA KATA MBILI ZA MRIJO NA MONDO


Mkuu wa Wilaya ya Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akimsikiliza diwani wa kata ya Mondo maelezo yake juu ya ujenzi wa mabweni ya shule ya sekondari Mondo.


 Mkuu wa Wilaya ya Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akikagua  mabweni ya shule ya sekondari ya Mondo.

 Wananchi wa kijiji cha Nkulali pamoja na wananchi wa kijiji  cha Mapango wakiwa katika  mkutano wa pamoja wa kutafuta suluhu baina ya mgogoro wa  matumizi ya ardhi baina ya vijiji hivyo viwili.

Mkuu wa Wilaya ya Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akikagua  mabweni ya shule ya sekondari ya Mondo.
     ................................................................

Na Shani Amanzi,
Mkuu wa Wilaya ya Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga amewataka Viongozi wa Serikali za Mitaa pamoja na Wazazi kuona umuhimu wa kuwapeleka watoto shule kwa ajili ya faida ya baadae na kutafuta suluhu ya namna watakavyoweza kuboresha miundombinu ya shule zao katika kutoa elimu.
Mhe. Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Chemba,Wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chemba  katika ziara yake ya siku moja katika kata mbili ya Mrijo na Mondo katika tarafa ya Goima Wilayani Chemba tarehe 29/12/2017.
Aidha Mhe Odunga amesema kumekuwa na migogoro mingi baina ya Serikali pamoja na Wananchi katika shughuli za kimaendeleo hasa makundi yanayopinga maendeleo kwa kuungana na Viongozi wa Serikali pamoja na wale ambao wanataka maendeleo na kuungana na baadhi ya Viongozi wa Serikali.
‘Na kutokana na hali hiyo inaleta mkanganyiko baina yao na kusababisha maendeleo kuchelewa mfano hai ni huu wa malimbikizo ya madeni toka 2013 katika ujenzi wa Shule ya Sekondari Mondo ambapo inatokana na hali ya kutoelewana’aliyazungumza Mhe.Odunga alipokuwa katika kata ya Mondo 
Pia Mhe.Odunga aliwataka  Wananchi wa kijiji cha Nkulali kuishi vizuri na Wananchi wa kijiji cha Mapango  na kila mmoja  aheshimu sheria na kanuni za umilikaji wa ardhi kwani matumizi ya ardhi katika kijiji aidha ya malisho au kilimo ni kanuni na taratibu zinazopangwa na Wananchi wa kijiji husika ,kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya mwaka 1999 na sheria ya matumizi ya ardhi  namba 6 ya mwaka 2007.
‘Suala la kuingiliana katika maeneo ya shughuli za kijiji flani bila kufuata kanuni na taratibu za eneo husika ni kosa kisheria na ni vyema Wananchi wa kijiji cha Mapango  wanaoendelea kulima eneo la malisho ya Wananchi wa kijiji cha Nkulari ni vyema wakasitisha hizo shughuli na kuomba kupewa maeneo mbadala kwa ajili ya shughuli za kilimo kwa kufuata taratibu.
Naye Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Chemba Bw.Enock Mligo amesema kulikuwa na mgogoro wa matumizi ya ardhi toka mwaka 2014. 
‘Serekali ilifanya jitihada za kufufua upya mipaka ya vijiji hivi viwili na kurudishia alama za kudumu (beacons) kwa kufuata ramani mama za Wizara ya Ardhi za mwaka 2008. Hata hivyo alama ambazo ziliwekwa wakazi wa Mapango walizing’oa na imebainika kwamba eneo linalotumiwa na wakazi wa Mapango ni la kijiji cha Nkulari na limetengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo kwa mujibu wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji cha Nkulari.’
Ziara ya Mhe Odunga ilikuwa ni ya kata mbili   ambazo ni Mondo na Mrijo  katika tarafa ya Goima wilayani Chemba ikiwa na lengo la kutatua migogoro ya wananchi katika shughuli zao za kila siku za kimaendeleo.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania