CURRENT NEWS

Sunday, December 24, 2017

MWAKIBINGA ATOA MSAADA WA CHAKULA KWA YATIMA KWA NIABA YA THE BRAIN TEAM




Kiongozi wa Kundi la Whatsapp Group la The Brain Team James Mwakibinga ametoa Msaada wa Chakula katika Kituo cha Kulelea Watoto yatima Wanaoishi Katika Mazingira Magumu Cha Mwandaliwa kilichopo Mbweni Jijini Dar ,Akizungumza na Wana habari Mwakibinga Amewataka Watanzania kuacha Kuwa na Mioyo Migumu ya Kujitolea kwa Watu wenye Mahitaji Maalumu  huku Watanzania wengi wakiendekeza anasa,na Kuchangia Michango Ya sherehe mbalimbali kwa Sifa ikiwemo Harusi huku Watu waishiyo Mazingira Magumu wakiteseka ,Mwakibinga Kwa niaba ya THE BRAIN TEAM  wametoa Mchele,Maharage,Mafuta ya Kupikia,Mbuzi Mmoja,Katoni za Juisi.
Akishukuru Kwa niaba ya Watoto hao Mama mlezi wa kituo hicho Amemshukuru Mwakibinga kwa niaba ya The Brain Team,huku akiwaomba wadau wengine Wasaidie Vifaa vya Shule kwa Watoto hao kipindi cha Januari Wakati Shule zikifungulia..
#Sisi ni TAIFA moja ,SISI NI TANZANIA MPYA
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania