Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akisaini Kitabu cha wageni katika Kituo cha Ihanje wakati wa ziara yake Wilayani Ikungi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Tatu kushoto) akimskiliza Mhandisi wa Ujenzi Sembua Mrisho wakati wa ukaguzi wa Jengo la upasuaji linalojengwa katika Kituo cha Afya Ihanje.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo (mbele) akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu pamoja na Mbunge wa Singida Magharibi Mhe. Elibariki Kingu wakiongozwa na Mhandisi wa Majengo kukagua ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Afya inayojengwa katika Kituo cha Afya Ihanje kilichopo Ikungi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akifurahi jambo na Mbunge wa Singida Magharibi Mhe.Elibariki Kingu wakati wakikagua ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Kituo cha Afya Ihanje.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Kulia) akikagua Ujenzi wa Kichomea Taka katika kituo cha Afya Ihanje.
............................................................................................................................
Nteghenjwa,Hosseah,Ikungi-Singida.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Mhe.Selemani Jafo amepongeza kazi
nzuri ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayoendelea kujengwa katika
Kituo cha Afya Ihanje kilichopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoani
Singida.
Mhe.Jafo alitoa pongezi
hizo wakati wa ziara yake Wilayani humo ya kukagua miradi ya maendeleo na
kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ambapo akiwa kituoni hapo alisema
ameridhishwa na usimamizi, ubora na maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya
Ihanje.
Aliongeza kuwa Kituo cha
Ihanje ni miongoni mwa Zaidi ya Vituo 200 vitakavyopekea/vilivyopokea
Fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Afya ambayo ilikosekana hapo awali
na kukifanya kituo hiki kutotoa huduma ipasavyo na agizo langu la awali ilikua
kumaliza kazi ya ujenzi mnamo Dec 30,2017 lakini kwa Ikungi walichelewa kuanza
utekelezaji kutokana na kupokea maelekezo mengine baadae ila wamefanya kazi
nzuri hivyo wao watakamilisha Jengo hili mnamo January 2018.
Nimekagua majengo yote sita
yanayojengwa kupitia uboreshaji huu hakika yanavutia na kupendeza, kuanzia
Maabara, Wodi ya Kinamama, Chumba cha Upasuaji, Chumba cha kuhifadhia Maiti
pamoja na kichomea Taka na ukizingatia ujenzi huu umewahusisha mafundi
kutoka kwenye Vijiji na Kata zetu ambapo kwa kuwatumia wao gharama za
ujenzi hupungua ukilinganisha na wakandarasi; Hii inanipa faraja
kubwa kuona kazi zinaenda vizuri kutoka kwa watalaam walioko kwenye jamii yetu,
Alisema Mhe.Jafo.
Awali akitoa taarifa hiyo
Mhandishi wa Ujenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Sembua Mrisho
amesema Fedha zilizopokelewa ni Tsh. Mil 720 kati ya hizo Mil 220 zimepelekwa
bohari ya dawa kwa ajili ya vifaa Tiba na Dawa mara majengo hayo
yatakapokamilika na Tsh Mil 500 ndizo zinazotumika katika Ujenzi wa miundombinu
yote sita na hali ya ujenzi mpaka sasa inaonyesha Fedha hizo zitakamilisha
kabisa mradi huo kwa ubora unaotakiwa.
“Mara baada ya kupokea
Fedha hizo na kupata Muongozo toka OR-TAMISEMI, Fedha zile zililetwa kwenye
Kata na zikaundwa kamati Tatu ya Mapokezi, Manunuzi na Ujenzi na kazi yote hii
imefanyika kwa kutumia “Local fund” na inasimamia na Wakandarasi wa
Halmashauri kwa kushirikiana na kamati za Ujenzi zilizopo” alisema Mrisho.
Akizungumza wakati wa Ziara
hiyo Mbunge wa Ikungi Mhe.Elibariki Kingu amesema Ihanje ni Kata pia ni Makao
Makuu ya Tarafa ya Ihanje na mradi huu umejibu shida za wananchi wa Ihanje na
Ikungi kwa Ujumla kwa sababu Kituo hicho kinatoa huduma kwa wakinamama wengi wa
Kata zaidi ya Tano zinazonguka eneo hili.
Aliongeza kuwa Kituo
cha Afya kilichkuwepo awali kilikuwa hakikidhi mahitaji kutokana na
kutokua na maeneo muhimu kama wodi nzuri na kubwa ya kina mama, maabara, sehemu
ya kuhifadhia maiti nk lakini kwa sasa sisi wananchi wa Ikungi tunaishukuru
sana Serikali yetu kwa kututatulia hangamoto hii.
Akizungumza kwa furaha
Angelina Naaman(Mama Yasinta) amesema “Wakinana mama sasa tutaona raha Zaidi ya
kujifungua kwa sababu tumepata mpaka chumba cha Upasuaji wakati awali ilikua
ukishindwa kujifungua kawaida inakua mtihani sana kwako na kwa wauguzi wenyewe
hivyo sasa zoezi la kujifungua kwetu litakua salama Zaidi kwa masiah yetu nay a
mtoto.
Ukarabati sambamba na
uboreshaji wa vituo vya Afya vinavyoendelea Nchini Kote utafanyika katika awamu
na awamu ya kwanza ilianza Mwezi Sept 2017 na utakamilika January, 2018 na
umehusisha vituo 44 wakati awamu ya Pili itaanza mwenzi January 2017 utahusisha
Vituo vya Afya 161.
Post a Comment