CURRENT NEWS

Sunday, January 21, 2018

DITOPILE ATOA SOMO KWA VIONGOZI WA CCM KATA.

    

 Mbunge wa viti maalum Mariam Ditopile akizungumza na wajumbe wa baraza la UVCCM kata ya Chang'ombe mkoani Dodoma wakati akifungua kikao cha baraza hilo na kukabidhi samani kwa ajili ya ofisi za CCM ngazi ya matawi katika kata hiyo.

 Mbunge wa viti maalum Mariam Ditopile akifungua kikao cha baraza la UVCCM kata ya Chang'ombe.


Wajumbe wa kikao cha baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM)kata ya Chan’gombe mkoani Dodoma 

    .....................................................................................................................................

MBUNGE wa viti maalum Mariam Ditopile amefungua kikao cha baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM)kata ya Chan’gombe mkoani Dodoma na kuwataka viongozi kutatua changamoto za wananchi ikiwa ni namna mojawapo ya kusafisha njia kuelekea chaguzi zinazokuja.

Aidha amewataka wenyeviti wa mtaa kuhakikisha uchaguzi wa serikali za mitaa unaokuja hawapotezi mtaa hata mmoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kura zitakazopatikana ziongezeke zaidi ukilinganisha na uchaguzi uliopita.

Mheshimiwa Ditopile amesema uchaguzi ulishamalizika kilichopo sasa hivi ni kwa viongozi kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ili chama kiendelee kuaminiwa na kupendwa na wananchi.

“Sisi wabunge wa viti maalum kazi yetu ni kuhangaika na utekelezaji wa Ilani maana nafasi zetu zimepatikana kutokana na wingi wa kura tulizopata katika mkoa wetu hivyo hatutalala tutahakikisha changamoto na kero za wananchi zinatatuliwa,

“Wenyeviti wa mitaa nyinyi ndio jeshi letu hakikisheni uchaguzi wa 2019 wa serikali za mitaa hatupotezi mtaa hata mmoja,kwenye makosa tujirekebishe ,diwani hakikisha hatupotezi mtaa wowote hapa,na katika uchaguzi mkuu tunataka kura ziongezeke kutoka zile zilizopatikana kwenye uchaguzi uliopita,”alisema mbunge huyo.

Amewataka viongozi kusema mambo mazuri ya kimaendeleo yanayofanywa na serikali na pia wahakikishe wanasimamia asilimia 5 ya vijana inafika kwa walengwa ili waweze kukopeshwa.

“Ni aibu kwa kiongozi wa CCM kukosa ajenda ya kuzungumza mbele ya wananchi wakati serikali inafanya mambo mengi ya kimaendeleo,huko ni kutoitendea haki CCM,elezeni miradi inayotekelezwa,simamieni upatikanaji wa asilimia 5 hiyo ndio kazi yenu,”alisisitiza Ditopile.

Katika mkutano huo mbunge huyo anayewakilisha kundi la vijana alichangia matofali 500,mifuko ya saruji 10 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya kata pamoja na vifaa mbalimbali vya matumizi ya ofisi za matawi yote ya kata hiyo na kutoa kadi kwa wanachama wapya 200 wa jumuiya hiyo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania