CURRENT NEWS

Sunday, January 7, 2018

DKT KALEMANI AKAGUA MAENEO AMBAYO WAZIRI MKUU ATAWEKA JIWE LA MSINGI

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametembelea maeneo mawili anayotarajiwa kuwekewa jiwe la msingi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tarehe 7/01/2018 katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Mradi wa kwanza aliotembelea ni wa jengo la Tanesco Mkoa wa Ruvuma lililoanza kujengwa mnamo mwaka 2014 ambao ulitarajiwa kukamilika mwishaoni mwa mwaka jana na kushindikana kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Mkandarasi.
Aidha mradi wa jengo hilo unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu na kuanza kutumika rasmi.
Pamoja na kutembelea jengo hilo la Ofisi ya Tanesco Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Kalemani alitembelea eneo kunakojengwa mitambo ya kupoozea umeme katika mradi mkubwa wa kusafirisha umeme wa Makambako Songea uliopo wilayani Songea mkoani Ruvuma ambako alijadiliana na wataalamu na kuweka baadhi ya vitu sawa tayari kwa ajili ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kuweka jiwe la msingi.
Meneja wa Mradi Mkubwa wa Usafirishaji wa Umeme wa Makambako - Songea Mhandisi Didas Lyamulya akitoa maelezo ya mradi kwa Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alipotembelea eneo la ujenzi wa mitambo ya kupoozea umeme unaoendelea kujengwa wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirirka la Umeme Tanzania (Tanesco) akieleza jambo mbele ya wajumbe walioambatana na Waziri wa Nishati ili kukagua eneo litakalowekwa jiwe la msingi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika eneo la ujenzi wa Mitambo ya Kupoozea Umeme katika mradi wa Kusafirisha umeme wa Makambako Songea.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (wa kwanza kushoto ) akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme katika mradi wa Kusafirisha Umeme wa Makambako-Songea wilayani Songea tayari kwa ajili ya kuwekwa kwa jiwe la msingi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kesho Tarehe 7/01/2018.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania Dkt. Tito Mwinuka akimweleza jambo walipotembelea eneo la uzinduzi wa mradi wa kusafirisha umeme wa Makambako-Songea ili kujionea maandalizi ya uzinduzi huo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania