CURRENT NEWS

Wednesday, January 3, 2018

'HAKUNA KITONGOJI KITAKACHOACHWA BILA UMEME NCHINI'-MGALU


Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza na wananchi alipokuwa akimkaribisha Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza na wananchi 

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akizungumza na wananchi 

                        ......................................................................................... 
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu amewaambia wananchi wa Kata ya Kiwangwa katika jimbo la Chalinze kuwa serikali imedhamiria kupeleka nishati ya umeme kwa wananchi na hakuna kitongoji kitakachoachwa bila kupatiwa huduma hiyo nchini.

Naibu Waziri huyo ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata hiyo alipokaribishwa na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete azungumze na wananchi wa kata hiyo kuhusu Mipango ya Kupeleka Nishati ya Umeme Vijijini. 

Mgalu amewaambia wananchi wa kata hiyo haswa katika vitongoji kuwa hakuna kitongoji kitakachoachwa bila kupatiwa umeme hasa maeneo yenye mahitaji maalum kama Hospitali, shuleni na kwenye shughuli za Kijamii kama Ofisi za kuhudumia wananchi.


Katika mkutano huo, pia Naibu Waziri huyo amefafanua juu ya taarifa za kuwepo na mabadiliko ya gharama za uunganishwaji wa umeme kutoka Sh.27,000 hadi Sh.180,000 ambapo amesisitiza kuwa hakuna mabadiliko yeyote. 
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania