CURRENT NEWS

Tuesday, January 16, 2018

HALMASHAURI NA MIKOA TENGENI MAENEO KWA AJILI YA WAJASIRIAMALI: DKT.NDUGULILE.

     
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akisalimiana na wanawake wajasiriamali wa kikundi cha Mafanikio kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mbozi wakati wa ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki kazi za maendeleo.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia bidhaa ya sabuni ya kuosha mikono wakati alipotembelea Kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Mafanikio kilichopo Manispaa ya Mbozi, mkoani Songwe, katika ziara ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.


Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia bidhaa ya Asali wakati alipotembelea Kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Maranatha kilichopo katika Manispaa ya Mbozi alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo mkoani Songwe.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiangalia bidhaa ya kahawa wakati alipotembelea Kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Mbozi Beach kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mbozi alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wanaachi kushiriki shughuli za maendeleo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akizungumza na mtoto katika moja ya ziara yake ya kutembelea Kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Mafanikio kilichopo kata ya Mlowo, Manispaa ya Mbozi, mkoani Songwe, alipofanya ziara ya siku mbili ya kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.

Mwakilishi wa Ofisi ya Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Bw. Yolla Ludege kutoka Kanda za Juu Kusini akitoa maelezo kuhusu taratibu za kukagua na kutoa vibali kwa wanawake wajasrliamali kutengeneza bidhaa zao wakati wa ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) mkoani Songwe iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.


Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi akielezea maana na umuhimu wa Kikundi Mlezi kwa wanawake wajasiliamali wa Mkoa wa Songwe wakati wa ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbozi Bi Tusubilege Benjamin akitoa neno kwa niaba ya Uongozi wa Wilaya kwa Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) kuhusu utekelzaji wa uwezeshwaji wa wanawake wakati wa ziara ya siku mbili ya Naibu Waziri huyo mkoani Songwe iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.


Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akizungumza na wanawake wajasiliamali walioshiriki kikao cha siku moja katika mji wa Vwawa, mkoa wa Songwe huku akiwa ameshika moja ya bidhaa zinazotengenezwa na wajasiriamali hao wakati wa ziara yake iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akitoa motisha kwa Vikundi ‘walelewa’ chenye mtaji mdogo na kuwaunganisha kwa ‘Vikundi Mlezi’ ambacho mtaji wake umeimarika ili waweze kusaidia katika kukuza biashara zao wakati wa ziara yake ya siku mbili Mkoani Songwe iliyolenga kuamsha ari ya wananchi kufanyakazi za maendeleo.


Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa ya “Songwe Coffee” katika mkoa wa Songwe wakati wa ziara yake kuamsha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
 .........................................................................

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) amezitaka Halmashauri na Mikoa kutenga maeneo kwa ajili ya wajasiriamali wadogowadogo ili kuweza kutatua changamoto zao na kuwawezesha kupata mbinu mbalimbali za kufanikisha matarajio yao na kupata maendeleo.

Ameyasema hayo Mkoani Songwe wakati akiitambulisha  Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ katika manispaa ya Mbozi yenye lengo la kuwawezesha wanawake wajasirimali kuwezeshana  kati yao wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza miradi ya biashara.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo linaenda sambamba na utendaji wa pamoja kwa kushirikisha uongozi wa Mikoa, Halmashauri na wananchi wenyewe katika kuibua miradi na kuanzisha shughuli za uzalishaji kwa kuzingatia matumizi ya fursa na weledi wa wananchi wenyewe.
  
Dkt.Ndugulile amesema kuwa ili kufanikisha kufikiwa kwa Tanzania ya viwanda Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali wadogo wadogo hasa wanawake kuwaweza kuanzisha vikundi vitakavyoanzisha viwanda vidogo vidogo na kuzalisha bidhaa zitakazo uzwa ndani na nje ya mkoa wa Songwe na hivyo kuutangaza mkoa kupitia bidhaa zilizozalishwa kwa kutumia ubunifu na rasilimali zilizopo.

Ameongeza kuwa lengo la kuzindua Programu ya ‘Kikundi Mlezi’ ni kuwashirikisha wanawake wajasiriamali waliokomaa katika biashara kuwasaidia wanawake wajasiriamali wanaoanza shughuli hizo kwa kuwapatia ujuzi, mbinu, maarifa, taarifa za soko na upatikanaji wa mikopo na vifaa.

“Niseme kutenga maeneo kwa ajili ya wajasiriamali wadogo ni muhimu kwenu wanawake wajasiriamali na hata wale ambao wanaanza na kwa asilimia kubwa itasaidia kuibua wanawake ambao hawakuwa na sehemu za kufanya shughuli zao pamoja na kuwawezesha kuanzisha biashara zao na kufanya wanawake kujiunga na vikundi na hatimaye kuanzisha viwanda vidogo na vya kati”alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile amesisitiza umuhimu wa kuamsha ari ya wananchi kufanya kazi kwa kuzielewa na kuziongezea nguvu juhudi zinazofanywa na Maafisa Maendeleo ya Jamii katika kuraghibisha jamii kujiletea maendeleo yao na hivyo kuzitaka mamlaka husika kuwawezesha wataalam hao kuwafikia wananchi kwa ajili ya kuwashirikisha kupata majawabu ya changamoto zilizopo.

Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bw. Julius Mbilinyi  amesema kuwa Wizara itaendelea kuhamasisha wanawake kujitokeza na kujiunga na vikundi na kusaidiana katika kuendesha biashara na kusaidia kuhamasisha Halmashauri kutenga asilimia 10 kwa wanawake na vijana ambazo zitatumika kama mtaji wenye masharti nafuu wa kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake Mweyekiti wa Halmashauri ya Mbozi Bw. Erick Mika  amesema kuwa programu ya ‘Kikundi Mlezi’ itasaidia kuwainua wanawake ikiwa halmashauri zinatenga maeneo mahususi kwa ajili yao hivyo kufanya wanawake kujitokeza kwa wingi kujishughulisha na shughuli za uzalishaji na kumuahakikishia Naibu Waziri kushirikiana na Maafisa Maendeleo ya Jamii katika kufanikisha masuala ya maendeleo katika Mkoa wa Songwe.

Mmoja wa Wanawake wajasiliamali Manisapaa ya Mbozi  Bi. Enea Mwanja ameishukuru Serikali kwa kuzindua Mpango huo utakaowawezesha wanawake kusaidiana  katika kuanzisha na kuboresha biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) anafanya ziara ya siku mbili mkoani Songwe kwa kuwatembelea wanawake wajasiliamali katika kuhamasisha wanawake kujishughulisha ili kusaidia kuchangia lengo la kuanzisha biashara ndogo na za kati kwa manufaa ya Taifa. Msisitizo umetolewa kwa wananchi kupenda kununua bidhaa zetu wenyewe ili kufikia lengo la uanzishaji wa viwanda 100 kwa kila mkoa. Tusiseme hatuwezi, tujipange kuanzisha na kubaini bidhaa zilizozalishwa mkoani Songwe ambazo zitatuwezesha kubaini idadi ya viwanda vilivyopo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania