CURRENT NEWS

Saturday, January 6, 2018

JAFO AACHA KICHEKO KWA WAFANYABIASHARA WA MABIBO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wafanya biasra wa Mabibo kwenye Mkutano uliofanyika katika Soko hilo kuhusu mauafaka dhidi ya mgogoro uliopoa baina ya wafanyabisara hao na Kiwanda cha Urafiki.

Wafanyabiashara wa Mabibo wakimskiliza Mhe.Waziri Selemani Jafo

Wafanyabisara wa Mabibo wakifuatilia Mkutano wa Waziri Jafo kuhusu suluhisho la wao kuondolewa katika kiwanja cha Soko hilo.
  

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Selemani Jafo akizungumza na wafanya biasra wa Mabibo kwenye Mkutano uliofanyika katika Soko hilo kuhusu mauafaka dhidi ya mgogoro uliopoa baina ya wafanyabisara hao na Kiwanda cha Urafiki.

   .................................................................
Nteghenjwa Hosseah, Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amekutana na wafanyabiashara wa Soko la Mabibo Jijini Dar es Salaam na kuzungumza nao kuhusu Tamko lililotolewa la kuwataka kuhamishwa na kuachia eneo hilo ambalo ni liko chini ya miliki ya Kiwanda cha Urafiki.


Waziri Jafo amefika katika eneo hilo baada ya kupata malalamiko kupitia Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kwamba wanataka  kutolewa kwa sababu kiwanja hicho sio kiwanja cha Soko halali na Mahakama imetoa hukumu ambayo inaonyesha eneo hilo liko chini ya Miliki ya Kiwanda.

Amesema dhamira ya serikali ni kuwajali wanyonge na kwamba wanaangalia namna ya kuwasaidia ili waweze kuendesha maisha yao.

“Sisi hatuna Mamlaka ya kuvunja hukumu ya Mahakama lakini katika hili kuna maslahi mapana ya wafanyabiashara ambao ni wanyonge wanaofanya biashara katika eneo hili lazima tuwaangalie kwa namna tofauti na kuangalia namna ya kuwasaidia ili waweze kuendesha maisha yao”amesema

Amesema kuwa Agenda ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli ni kuhakikisha wanyonge wanapata haki zao hivyo amemuagiza afike kuwasikiliza na kutafuta suluhisho la haraka dhidi ya wafanyabiashara wa Mabibo.

“Baada ya kufika hapa nimetoa agizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda kukutana na Yono Auction Mart, Uongozi wa Kiwanda na wote wanaohusika ili tupate njia muafaka ya kuhakikisha wafanyabishara wa eneo hili wanaendelea kufanya biashara zao vizuri kama walivyokuwa wanafanya hapo awali”amesema Jafo

Amewaomba kuwa watulivu waendelee  na biashara zao wakati serikali  inalishughulikia kwa umakini na haraka zaidi.

"Ukizingatia hiki ni kipindi cha mwezi Januari ambapo Fedha zinahitajika kwa ajili ya ada za watoto, kodi za nyumba nk mkibugudhiwa mtashindwa kukidhi mahitaji ya Familia,"amesema Jafo.

Soko la Mabibo lenye wafanyabiashara zaidi ya 2000 limekumbwa na mgogoro huo kwa miezi kadhaa iliyopita kufuatia Kiwanda cha Urafiki kuwataka waondoke hapo ili kupisha eneo hilo kwa matumizi ya kiwanda.

 Hata hivyo eneo maalumu la kuwahamishia wafanyabiashara hao bado halijakamilika lakini pia wafanyabishara wamekuwa wakionyesha hisia zao kuwa eneo hilo walilopo sasa ni la Kimkakati kwa  biashara zao kutokana kuwa katikati ya Mji na ni rahisi  kufika kwa wateja wa aina zote.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania