Ujenzi wa jengo la upasuaji linaloendelea katika Kituo cha Afya Karume wilayani Rombo
Jengo la wodi ya wazazi inayojengwa katika kituo cha Afya Karume.
.................................................................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo
ameonyesha kukerwa na kutoridhishwa na kasi ya utendaji kazi wa Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Rombo na watendaji wake wa chini kwa kushindwa kwenda sambamba
na kasi anayoitaka katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Hali hiyo ilijitokeza leo wakati Jafo alipokuwa katika ziara
yake ya kukagua miradi ya maendeleo iliyopo mkoani Kilimanjaro.
Amesema Halmashauri ya wilaya ya Rombo ni miongoni mwa
Halmashauri zilizopokea fedha za awamu ya kwanza ya uboreshaji vituo vya afya
lakini licha ya kupokea fedha hizo tokea mwezi Agosti mwaka 2017 bado wapo
nyuma ukilinganisha na halmashauri zingine zilizopata fedha kwa wakati mmoja.
Akikagua kituo cha afya Karume , Waziri Jafo amemtaka mkurugenzi
wa Halmashauri hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuwapa ushirikiano
wa kutosha watendaji walio chini yake ili waweze kumaliza kazi hiyo kabla Februari
25, mwaka huu.
Kadhalika, Jafo amewapongeza Mkuu wa wilaya ya Rombo Agness Hokololo
na Katibu Tawala wake wa wilaya Asenga kwa kazi kubwa wanayofanya ya kusimamia
maendeleo ya wilaya hiyo.
Post a Comment