CURRENT NEWS

Monday, January 8, 2018

JAFO APONGEZA JITIHADA ZA MBUNGE WA MAKAMBAKO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo(Katikati) alipotembelea Hospital ya Mji wa Makambako.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akisalimia na Muuguzi wa Hospital ya Mji wa Makambako alipotembelea Hospital hiyo kukagua utoaji wa uduma za Afya 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe.Lucy Msafiri wakati wa ziara yake katika Hospital ya Mji wa Makambako. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo katika Picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya pamoja na watumishi wa Hospital ya Mji wa Makambako. 

Huu ndio Muonekano wa Hospital ya Makambako unavyoonekana kwa hivi sasa

    ................................................................

Nteghenjwa Hosseah,Makambako.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amempongeza Mbunge wa Makambako Mhe. Deo Sanga kwa jitihada mbalimbali anazozifanya katika kuboresha Sekta ya Afya katika Jimbo hilo.

Jafo ameyasema hayo wakati alipotembelea Hospital ya Mji wa Makambako na kuona vyumba viwili vya Madaktari ambavyo vimejengwa na Mbunge Mhe. Sanga.

"Kwa dhati kabisa nimpongeze Mhe. Sanga kwa kujitoa kuboresha huduma za Jamiia hii inaonyesha nia yake njema katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa sabababu wananchi wakiwa na Afya Njema wataweza kuendelea na shughuli zao kikamilifu za kujitaftia kipato kisha kupata maendeleo" Alisema Jafo

Kwa kutambua Idadi kubwa ya watu wanaopata huduma katika Hospital hiyo ambayo ina miundombinu Duni ikiwa ni pamoja na ukosefu wa Jengo la kisasa la Kuhifadhia Maiti pamoja na Ukosefu wa wodi mbalimbali.

Waziri Jafo amesema  Serikali itaangalia jinsi ya kuboresha miundombuni hiyo ili wakazi wa Makambako waweze kupata huduma bora za Afya kama Watanzania wanazopata wengine.

"Tutaweka Jitihada katika kutafuta Fedha kutoka kwenye vyanzo vyetu Ili kuongeza miundombinu ya Afya na hospital hii iweze kuwa na hadhi ya kuwa na Hospital ya Mji" Alisema Jafo.

Hata hivyo Jafo amechukua  kilio cha Hospital hiyo kuendelea kupata mgao wa Kituo cha Afya wakati imeshapandishwa hadhi kuwa Hospital ya Mji ana ameahidi kulishughulikia.

"Makambako ni eneo muhimu sana katika Kanda hii yenye wakazi wengi, shughuli nyingi za kiuchumi na muingiliano wa watu wengi kutoka ndani na nje ya Nchi hivyo inahitaji huduma bora zaidi za Afya kwa kwa kuzingatia  umuhimu wa eneo na wananchi wake" alisema Jafo.

Waziri Jafo anaendelea na ziara yake katika Mikoa Mbalimbali lengo ni ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo iki chini ya Ofisi ya Rais Tamisemi. 


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania