CURRENT NEWS

Thursday, January 25, 2018

JAFO ATAKA MAJI YAPATIKANE SHULE YA SEKONDARI KONDOA


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akikagua miundombinu ya Bweni katika shule ya Sekondari ya Wasichana Kondoa.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akikagua vyoo vya shule ya Wasichana Kondoa ambavyo viko katika hali mbaya.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) alishiriki kifungua kinywa (Uji) katika Jiko la Shule ya wasichana Kondoa.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akikagua Chumvi inayotumika kupikia wanafunzi wa Kondoa kama ina madini Joto.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Mchepuo wa Sayansi(PCM).

    .........................................................................................

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kupeleka Miundombinu ya Maji katika Shule ya Wasichana Kondoa Sekondari.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara yake Wilayani humo na kukagua Majengo ya Sekondari Kondoa kabla ya Ukarabati Mkubwa unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

“Nimekuja leo katika Shule hii kwanza kukagua uchakavu wa majengo wanayotumia watoto wetu, kuzungumza na wanafunzi na kusikia kutoka kwa Mhandisi Mshauri kile wanachotarajia kufanya katika kazi ya ukarabati waliyopewa,”amesema Jafo.

Waziri Jafo alisema kuwa “Katika Ukaguzi wangu nimegundua uchakavu wa Mabweni, Ofisi za Walimu, Madarasa, bwalo, Jiko lakinI zaidi nimegundua uchakavu wa vyoo na ukosefu wa maji katika Shule hii”

Ameongeza kuwa Uchakavu wa vyoo ni hatari kwa maisha ya wanafunzi na wakati wowote unaweza kusababisha matatizo na pia ukosefu wa maji ndio unazidi kuvifanya vyoo kuwa hatari Kiafya na kuonekana vichafu zaidi.

“Nasisitiza katika Ukarabati unaoanza Muanze na vyoo na vijengwe upya na wala sio kukarabati hivi vya zamani.Maji ni kitu muhimu sana katika shughuli zetu za kila siku na katika suala la usafi maji ni muhimu sana na wanafunzi hawa wako zaidi ya mia tano,”amesema

Amebainisha kuwa kukosekana kwa Maji kunasabisha uchafuzi wa mazingira na kuhatarisha Afya zao, hivyo Kumtaka Mkurugenzi wa halmashauri ya Kondoa kuhakikisha maji yanatoka shuleni hapo.

“Nataka nikirudi hapa Mwezi wa Tano nikute maji yanatoka, vyoo vipya sambamba na Ukarabati ulioanishwa, “amesisitiza Jafo.


Kadhalika, katika kikao chake na wanafunzi wa shule hiyo walimuahidi Waziri jafo matokeo mazuri katika mtihani wa kidato cha sita utakaofanyika mwaka huu na kusema kuwa watafanya vizuri na alama za mwisho kwa mwanafunzi zitakuwa daraja la II.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania