CURRENT NEWS

Wednesday, January 3, 2018

JAFO,PROF.MAJI MAREFU WAUNGURUMA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA KWAGUNDA KOROGWE.

       

 1.       Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akimnadi Mgombea udiwani wa Kata ya Kwagunda(CCM) Saidi Athumani maarufu kwa jina la Moto.
    Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani  akizungumza katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kwagunda
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kwagunda
 Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kwagunda
Umati wa wananchi waliokuwepo kwenye kampeni za udiwani kata ya kwagunda
     ..............................................................................................................................
KAMPENI za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kwagunda wilayani Korogwe zimeendelea kushika kasi ambapo leo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo na Mbunge wa Korogwe vijijini Stephen Ngonyani maarufu kwa jina la Prof. Maji marefu wameunguruma kumnadi mgombea wa CCM  Saidi Athumani.

Uchaguzi umetokana na aliyekuwa diwani wa kata hiyo kufariki dunia miezi michache iliyopita.

Katika kampeni hizo, Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe ndiye aliyekuwa mgeni rasmi akiwa na mwenyeji wake  Prof. Maji marefu wamewaeleza wananchi kwamba watumie fursa hiyo kuhakikisha januari 13 mwaka huu hawafanyi makosa wamemchague Saidi ili aweze kuwatumikia ipasavyo.

Wamewataka wananchi kukiamini chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa chini ya Rais John Magufuli kimejipambanua kuwatumikia wananchi wanyonge na maskini.

Mkutano huo ulihudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi huku CCM ikidhihirisha imejipanga kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania