CURRENT NEWS

Wednesday, January 10, 2018

JIJI LA DAR ES SALAAM KUPOKEA TUZO YA HUDUMA BORA YA USAFIRI ENDELEVU  ....................................................
Nteghenjwa, Hosseah, Dar es Salaam.

Jiji la Dar es Salaam limechaguliwa kupata tuzo ya huduma bora ya Usafiri endelevu barani Afrika kufuatia Mradi wake wa mabasi yaendayo haraka (DART) ambao kwa kiasi kikubwa umeleta mabadiliko katika kutatua changamoto ya msongamano wa Magari uliokuwa ukiikabili Jiji la Dar es Salaam.

Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa Habari Waziri mwenye dhamana na Mamlaka ya Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amesema Jiji hili la Dar es salaam litapokea tuzo mapema leo tar 09 jan 2018 katika hafla itakayofanyika huko Nchini Marekani katika Jiji la Washington Dc kufuatia utoaji wa huduma huduma hiyo bora ya Usafiri.

“Huduma ya Usafiri katika awamu hii ya kwanza imeonyesha mafanikio makubwa kufuatia uwezo wa kupunguza muda wa kusafiri kwa wananchi kutoka masaa matatu waliyokua wanatumia hapo awali hadi kufikia kutumia dakika 40 kwa watumiaji wa Mabasi haya kutoka Kimara hadi eneo la Katikati ya Jiji la Dar es salaam” Alisema Jafo.

Jafo aliongeza kuwa Tangu kaunzishwa kwa Mradi huu wa Mabasi yaendeyo Haraka(DART) umetoa ajira kwa watanzania kwani zaidi ya watumishi 967 wamepata fursa za kutumikia Taasisi hii hivyo ni fursa pia ya kiuchumi kwa watanzania.

Zaidi hapo Mradi huu huathiri Mazingira kwani Injini zinazotumiwa na mabasi yaendayo haraka kutokuwa na athari kwenye mazingira, Mabasi haya hayotoa Moshi wala kusababisha kelele katika ya Mji hivyo mradi kuwa rafiki kwa  mazingira alisisitiza Jafo.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mabasi yanedayo haraka Victor Ndonne akizungumza katika kikao na waandishi wa habari alisema Ujumbe kutoka Tanzania katika halfa ya Upokeaji wa Tuzo hiyo Nchini Marekani unaongozwa na Balozi wa Tanzania katika Nchi za Marekani na Mexico Balozi Wilson Masiling ambaye ameambatana na Naibu Katibu Mkuu(E) kutoka OR-TAMISEMI Bw.Tixon Nzunda, Mwenyekiti wa Bodi ya DART pamoja na Mtendaji Mkuu wa DART.

Mradi wa abasi yaendayo Haraka unatekelezwa katika awamu sita ambapo ujenzi wa miundombinu katika awamu ya Pili ya Mradi katika Barabara ya Kilwa inataraji kuanza mapema mwaka huu.

Hii ni Tuzo ya pili kupokelewa na Wakala wa Mabasi yendayo haraka ambapo hivi  karibuni Taasisi ya C40 YA Marekani iliipa Jiji la Dar es salaam Tuzo ya Usafirishaji endelevu pamoja na Jiji la Newyork ka Marekani. 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania