CURRENT NEWS

Saturday, January 6, 2018

KAMPENI ZA CCM KATA YA KURUI KISARAWE ZAPAMBA MOTO.

Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo akimnadi Mgombea udiwani kata ya Kurui Kunikuni.

Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Pwani Zainabu Vullu na madiwani.
Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo akiwa na baadhi ya wanachama wa CCM katika kampeni za udiwani kata ya Kurui wilayani Kisarawe.

Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo akiwa na baadhi ya wanachama wa CCM katika kampeni za udiwani kata ya Kurui wilayani Kisarawe.
Wanachama wa CCM wakiwa na Mbunge wao Selemani Jafo

        ......................................................................

Kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kurui wilaya ya Kisarawe  zimeendelea kupamba  moto ambapo leo Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amemnadi mgombea wa udiwani kwa Kata hiyo Kunikuni huku akichambua utekelezaji wa ilani ya CCM.

Katika kampeni hizo, Mhe. Jafo amemnadi mgombea huyo kwa kuchambua utekelezaji wa Ilani ya CCM na kueleza mafanikio makubwa yanaendelea kupatikana katika sekta mbalimbali. 

Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na ujenzi uliomalizika na  unao endelea  wa madaraja sita  ya Kipora, Kologombe, Matulanga, kwakonzi, Kologombe, Muyombo, na Nyatanga.

 Pia Ujenzi wa barabara za lami kwa mji wa Kisarawe, kutangazwa kwa ujenzi wa barabara ya lami ya kilometa 8.2 kwa barabara ya Kisarawe hadi Maneromango, Ujenzi wa vituo cha afya Maneromango, chole, na Mzenga, ujenzi wa sekondari ya kidato cha tano Maneromango, ujenzi wa shule za Kwala, Mitengwe, Kitonga, na Boga yote ni baadhi ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM. 

Kutokana na mafanikio hayo yamewakuna wanachama kadhaa wa CUF  kujiunga na CCM wakati Jafo akiwa jukwaani.

Wanachama hao wameongozwa na mwenyekiti wa CUF Kata ya Kurui ndugu Shabani Maulidi ambao wamejiunga na CCM.

Jafo amewashukuru wanachama hao na amewaomba waungane pamoja kukipatia Chama Cha Mapinduzi ushindi wa kishindo hapo januari 13, mwaka huu.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania