CURRENT NEWS

Friday, January 12, 2018

MADEREVA BODA BODA WALA KIAPO CHA KUWALINDA WATOTO DHIDI YA MIMBA ZA UTOTONI MKOANI KATAVI.

Baadhi ya Madereva Boda boda wa Wilaya ya Mpanda wakiongozwa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) kula kiao cha uadilifu na ulinzi wa watoto wa kike dhidi vitendo vya ngono wakati alipofanya ziara ya siku mbili ya kuhamasisha kutokomeza mimba za utotoni katika kwa kutekeleza “Kampeni ya Mimi ni Msichana Najitambua Elimu Ndio Mpango mzima”.
Baadhi ya Madereva Boda boda wa Wilaya ya Mpanda wakiongozwa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) kula kiao cha uadilifu na ulinzi wa watoto wa kike dhidi vitendo vya ngono wakati alipofanya ziara ya siku mbili ya kuhamasisha kutokomeza mimba za utotoni katika kwa kutekeleza “Kampeni ya Mimi ni Msichana Najitambua Elimu Ndio Mpango mzima”.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akizungumza na madereva Boda Boda wa  Wilaya ya Mpanda mara baada ya kuwaapisha kuwalinda watoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni alipofanya ziara ya siku mbili ya kuhamasisha wananchi kupambana na mimba za utotoni katika mkoa wa Katavi.


 Baadhi ya madereva Boda Boda wa  Wilaya ya Mpanda wakiwa wanakisikiliza nasaha za Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) muda mfupi baada ya kuwaapisha kuwalinda watoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni ili kutimiza ndoto zao alipofanya ziara ya siku mbili ya kuhamasisha wananchi kupinga mimba za utotoni kupitia ,“Kampeni ya Mimi ni Msichana Najitambua Elimu Ndio Mpango mzima”.

Baadhi ya madereva Boda Boda wa  Wilaya ya Mpanda wakiwa wanakisikiliza nasaha za Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) muda mfupi baada ya kuwaapisha kuwalinda watoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni ili kutimiza ndoto zao alipofanya ziara ya siku mbili ya kuhamasisha wananchi kupinga mimba za utotoni kupitia ,“Kampeni ya Mimi ni Msichana Najitambua Elimu Ndio Mpango mzima”.


Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe.Lilian Masinga akihamasisha madereva Bodaboda wa  Wilaya ya Mpanda kushiriki jukumu la kuwalinda watoto wa kike dhidi ya mimba za utotoni mara baaada ya kuwaapishwa kuwalinda watoto hao waweze kunufaika na haki ya Mtoto kuendelezwa ili kutimiza malengo yao alipofanya ziara ya siku mbili ya kuhamasisha wananchi kutokomeza mimba za utotoni katika katika mkoa wa Katavi.


Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) akitoa cheti cha kwa kiongozi wa madereva Bodaboda wa Mkoa wa Katavi Bw. Salum Mwakambafu wakati wa ziara yake ya kuhamasisha wananchi kupambana na mimba za utotoni kupitia “Kampeni ya Mimi ni Msichana Najitambua Elimu Ndio Mpango mzima”.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
...........................................................

Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Madereva Bodaboda wa wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamekula kiapo cha uaminifu cha kuwalinda watoto wa kike dhidi ya vitendo vya ngono na mimba za utotoni zinazo sababisha kukatisha haki yao ya kuendelezwa.  

Kiapo hicho kimeongoza na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(Mb) ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa “Kampeni ya Mimi ni Msichana Najitambua Elimu Ndio Mpango mzima” iliyozinduliwa tarehe 11 Oktoba, 2017 kwa lengo la kuhamasisha wananchi kupambana na kuzuia matukio ya mimba za utotoni katika jamii zetu.

Dkt.Ndugulile amesema kuwa  ili kufanikisha kutokomeza mimba za utotoni hatuna budi kuweka ushirikiano baina ya wazazi, walezi, jamii, Serikali na wadau wengine ili kuwaepusha watoto wa kike kupata vishawishi vya mahusiano ya kingono katika umri mdogo na hatimaye kupata mimba za utotoni.

Ameongeza kuwa lengo la Kampeni ya “Mimi ni Msichana Najitambua Elimu ndio Mpango Mzima" imelenga kuunganisha nguvu za pamoja za wanajamii wakiwemo madreva wa Bodaboda kushirikiana na Serikali kuzuia na kutokomeza matukio ya mimba za utotoni katika ngazi ya jamii na shuleni.

“Niseme kampeni  hii itasaidia kwa asilimia kubwa kuunganisha nguvu zetu kama wananchi na sisi Serikali katika kutokomeza vitendo hivi viovu”alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile amewaasa madereva hao kuondokana na tamaa za kujihususha na mahusiano na kingono na watoto wadogo bali wao kuwa walinzi wao katika kutokomeza suala mimba kwa watoto wetu.

 Amewataka kufichua vitendo vyovyote vyenye ushawishi wa mahusiano yanayosababisha mimba kwa watoto wa kike ili Sheria iweze kuchukua mkondo wake.  

Kwa upande wake Mkuu wa  Wilaya ya Mpanda Mhe. Lilian Matinga amesema kuwa wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kwa kuweka mikakati ya kupambana na wanaume na vijana wakware wanaotumia fursa zao kuwa na mahusiano maovu na watoto wa kike katika Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi ambao ndio unaoongoza kitaifa kwa kuwa na asilimia 45.

Mmoja wa  dereva Boda boda wa Wilaya ya Mpanda Bw. Juma Salum kwa wakati tofauti wameishukuru Serikali kwa kuandaa Kampeni hiyo itakayowajengea uelewa wananchi kusaidiana  katika kuwalinda watoto wa kike kwa kuweka miundo mbinu salama ya kusomea na kujifunzia ili kupunguza kiwango cha mimba za utotoni kwa silimia 50 ifikapo mwak 2021/22.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) alikuwa na ziara ya siku mbili mkoani Katavi kuhamasisha wananchi kupambana na kuzuia mimba za utotoni kupitia “Kampeni ya Mimi ni Msichana Najitambua Elimu Ndio Mpango mzima”.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania