CURRENT NEWS

Friday, January 12, 2018

MAHENGE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMANDA WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI NCHINI NA KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA USALAMA BARABARANI TANZANIA SACP FORTUNATUS MUSILIMU..................................................
*KWA UFUPI YALIYOJIRI WAKATI MKUU WA MKOA WA DODOMA DKT. BINILITH MAHENGE ALIPOKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMANDA WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI NCHINI NA KATIBU MTENDAJI WA BARAZA LA USALAMA BARABARANI TANZANIA SACP FORTUNATUS MUSILIMU, JANUARI 11, 2018*

*#Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge* leo amekutana na kufanya mazungumzo na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Usalama Barabarani Tanzania SACP Fortunatus Musilimu hapa mjini Dodoma.

*#Viongozi hao* wamezungumza masuala muhimu yenye lengo la kuendelea kuboresha zaidi hali ya usalama barabarani hapa nchini.

*#Dkt. Mahenge:Ipo haja ya kuitazama Dodoma kwa jicho la kipekee na kuimarisha zaidi hatua mbalimbali za usalama barabarani kwa kuzingatia kuwa Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi, Serikali imeshahamia, idadi ya watu inaendelea kuongezeka kwa kasi na shughuli mbalimbali zinaongezeka.

*#Dkt. Mahenge:* Doria za Ulinzi na Ukaguzi barabarani ziongezeke hadi nyakati za usiku kucha kwa kuwa baadhi ya wahalifu hupendelea pia kufanya matukio ya kihalifu nyakati za usiku ambapo masuala ya ujangili, kupitisha magendo, madawa ya kulevya, uhamiaji haramu na masuala mengine hufanyika sana nyakati za usiku.

*# Dkt. Mahenge:* Nashauri Mkakati ujao upige kabisa marufuku tabia ya watu kuendesha vyombo vya moto wakiwa wamekunywa pombe jambo ambalo ni hatari na limesababisha athari kubwa kwenye baadhi ya Maeneo.

*#Dkt. Mahenge:* Baadhi ya Watu wamefanya mazoea tabia ya kutoka na vyombo vya usafiri vya moto na kwenda navyo maeneo ya burudani kunywa pombe na kisha kuendesha magari hayo wakati wa kurudi wakiwa wamekunywa pombe, mkakati mpya uelekeze kukomesha tabia hii.

*#Kamanda Musilimu:* Baraza limefikia hatua ya kufanya tathimini ya utekelezaji waMkakati wa kukabiliana na ajali za barabarani nchiniwa kipindi cha miezi sita kuanzia Julai 2017 hadi Disemba 2017 ambao kimsingi umemaliza muda wake ili kuweza kutengeneza Mkakati mpya

*#Kamanda Musilimu:* Tathimini hiyo itawezesha kubaini mafanikio na mapungufu yaliyopo kwenye Mkakati uliomaliza muda wake na kuwa tathimini hiyo ndio itasaidia kuandaa mkakati mpya utakao kuwa bora zaidi kuliko huu uliomaliza muda wake.

*#Kamanda Musilimu:* Mkakati unaofanyiwa tathimini ulikuwa umesheheni masuala mengi muhimu ambayo yalilenga kupunguza matukio ya ajali za barabarani kwa asilimia 10% kwa kipindi hiko cha miezi sita (Julai hadi Juni, 2017)

*#Kamanda Musilimu:* Mkakati uliomalizika muda wake wa kutekelezwa ulilenga kupambana na makosa yanayosababisha madhara makubwa kwenye ajali za barabarani, kuimarisha ukusanyaji, utunzaji na ukokotoaji wa takwimu za ajali za barabarani ili zisaidie katika mapambano ya ajali barabarani.

*#Kamanda Musilimu:* Mkakati pia ulilenga kuongeza nguvu katika utoaji elimu, mafunzo na uenezi katika suala la usalama barabarani. Aidha, Ulilenga kuimarisha mfumo wa usalama barabarani hapa nchini kwa kushirikisha wadau mbalimbali.

*#Kamanda Musilimu:* Mwisho Mkakati ulisisitiza dhana ya kulifanya suala la usalama barabarani kuwa Agenda ya Kitaifa na kupambana na rushwa na viashiria vyake dhidi ya ajali za barabarani.

*Imetolewa na:*

*OFISI YA MKUU WA MKOA* *DODOMA*
*Januari 11, 2018*
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania