CURRENT NEWS

Wednesday, January 3, 2018

MAVUNDE AAHIDI KULIPATIA UFUMBUZI SUALA LA FIDIA KWA WANANCHI WA MAKOLE

Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na wananchi wa Kata ya Makole

 Mbunge wa Dodoma mjini Anthony Mavunde akizungumza na wananchi wa Kata ya Makole
 Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao

    Wananchi wakimsikiliza Mbunge wao
              .....................................................................................................................

MBUNGE wa jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde amefanya ziara katika kata ya Makole na kuahidi kulipatia ufumbuzi suala la ulipwaji fidia kwa wananchi wanaopisha upanuzi wa Kiwaja cha Ndege cha Dodoma.

Mavunde amefanya ziara hiyo kwa lengo la kusikiliza kero zinazowakabili wananchi wa maeneo mbalimbali.

Katika ziara yake kwenye kata hiyo,Mavunde amesema atafuatilia na  kulipatia ufumbuzi suala la ulipwaji fidia kwa wananchi hao.

"Wananchi hawa wanapisha maeneo yao kwa ajili ya upanuzi wa Kiwanja cha Ndege,kurekebisha miundombinu ya barabara na kufungua barabara ambazo hazipitiki,kurekebisha mfumo wa majitaka eneo la Makole Kisiwani,Upatikanaji wa wodi ya wakina mama katika Kliniki ya Makole,"amesema

Aidha amewahakikishia wananchi juu ya upanuzi wa kituo cha Afya cha Makole kuwa kitakuwa cha kisasa kutokana na serikali kutoa ambapo kiasi cha Shilingi milioni mia tano (Tsh 500,000,000/=) kwa ajili ya kuboresha kituo hicho.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania