Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Dodoma wakiongozwa na
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.Binilith Mahenge wakitembelea eneo lilokumbwa na
mafuriko Chemba
Eneo lilokumbwa na mafuriko na kuzingira nyumba za wananchi
Eneo lilokumbwa na mafuriko na kuzingira nyumba za wananchi
.....................................................................................
Mvua kubwa zilizonyesha usiku wa kuamkia Januari 9, 2018
Wilayani Chemba Kata ya Mrijo mkoani Dodoma, zimesababisha athari kubwa
kwenye vijiji vitatu vya kata hiyo.
Vijiji vya Kata hiyo vilivyoathiriwa ni Mrijo Chini,
Kaloleni na Olboroti ambapo taarifa ya awali ya tathimini ya Wilaya ya Chemba ambapo
Takribani nyumba 1000 zimezingirwa na maji
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma inaonesha kuwa takribani Nyumba 70 zimedondoka ambapo kwa Elboroti-39,
Kaloleni-22, Mrijo Chini-9
Aidha taarifa ya Tathimini ya awali pia inaonesha Wananchi
walioathiriwa na mafuriko hayo wamepoteza mifugo na vifaa vya majumbani.
Wakizungumzia hali hiyo Wenyeji wa eneo hilo wamesema Hali kama
hiyo iliwahi kujitokeza miaka ya 1968 na kuwa sehemu hiyo ni eneo la mkondo wa
maji na kipindi hiko maji yakituama yalikuwa yakitumika kunywesha mifugo, lakini
baadae Wananchi wakagaiwa viwanja na kujenga.
Kadhalika, katika taarifa hiyo imeeleza kuwa Uongozi wa Wilaya
ya Chemba umelazimika kuzifunga shule mbili kwa Kuwa zimezingirwa na maji na
hivyo siyo sehemu salama kwa Wanafunzi, shule ya msingi kaloleni na shule ya
Sekondari Mrijo.
Imesema kuwa hakuna mtu aliyepoteza maisha kufuatia mafuriko
hayo na kwamba Tathimini ya Kina inaendelea kufanyika kubaini athari zaidi na
mahitaji halisi ya Wananchi wahanga ili kuweza kuwasaidia.
Hadi sasa wananchi wameopolewa kutoka eneo la mabondeni ambapo
maji yamezingira nyumba za Wananchi, na Wananchi wachache waliobakia Kazi ya
kuwatoa mabondeni kwenye maji kuwapeleka eneo la makazi yaliyopo maeneo ya
muinuko inaendelea Hadi kufikia usiku wa Januari 10.
Pia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma limewekwa Kambi
eneo Hilo kuhakikisha Wananchi wote wanatolewa eneo lenye maji na kupelekwa
eneo salama kwa Usalama huku Serikali imeandaa makazi eneo la shule kwa ajili
ya Wananchi wale watakaokosa hifadhi kwa ndugu jamaa na marafiki.
Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia kwa kushirikiana na Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Chemba Dkt. Mashimba wametoa mahindi Gunia 50 kwa
ajili ya kusaidia Wananchi hao wahanga na serikali ya Serikali hiyo imetenga
Maghala mawili kwa ajili ya kuhifadhia baadhi ya Mali za Wananchi
zilizofanikiwa kuopolewa kwenye eneo lililoathirika kwa maji.
Kufuatia Hali hiyo, MKuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge
akiambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma
wamefika eneo la tukio kuwajulia Hali Wananchi, kuwapa pole na kuona Hali
halisi ya athari zilizotokea.
RC Dkt. Mahenge amesisitiza Wananchi wa eneo la Mrijo Kuwa kitu
kimoja kushikamana na kusaidiana kwenye janga hili kwa Wananchi walio kwenye
makazi salama kusitiri wenzao wahanga
Ili kuhakikisha Usalama na kunusuru maisha ya Wananchi
kwenye waliokuwa wanaishi mabondeni, Dkt. Mahenge amewapiga marufuku
Wananchi hao wasirudi tena kwenye makazi yao kwa kuwa eneo hilo siyo
salama tena kwa Kuwa mvua zinaendelea kunyesha.
Mahenge amewaagiza wataalamu wa Wilaya ya Chemba kwenda kupima
eneo lililozingirwa na maji ili kubaini Wananchi wasiotakiwa kurudi tena kwenye
eneo Hilo la makazi.
Aidha amemwagiza Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na Wataalamu wa
Halmashauri ya Chemba kuwapimia Wananchi viwanja vipya vya makazi kwenye eneo
lililoinuka na salama kwa makazi ili Wananchi wajenge makazi mapya
Hata hivyo amesema Uharibifu wa Mazingira kama ukataji miti
hovyo ndio umeleta mabadiliko haya ya Tabia ya Nchi yenye athari kama hizo za
mvua na mafuriko, na kuagiza Kampeni ya Upandaji miti eneo hilo.
“ Nimeagiza Timu ya Wataalamu wa Afya wafike haraka eneo la
tukio na kuchukua hatua muhimu kuhakikisha wanazuia magonjwa yote ya mlipuko
yanayoweza kutokea, na athari zingine kiafya,”
Ameongeza “Naagiza Wakuu wa Wilaya Wote, Wakurugenzi wa
Halmashauri Wote, Makatibu Tarafa Wote na Wenyeviti wa Serikali za
Mitaa muhakikishe Wananchi wote wanaoishi mabondeni wanahama mara
moja kama tahadhari ya mvua zinazoendelea kunyesha hapa Mkoani
Dodoma.
Post a Comment