CURRENT NEWS

Wednesday, January 24, 2018

POLEPOLE, JAFO WAITEKA SANYA JUU KAMPENI ZA UBUNGE SIHA

 Viongozi mbalimbali wakifuatilia hotuba ya mgombea ubunge wa Jimbo la Siha Dk.Godwin Mollel
 Katibu wa  NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akimkaribisha jukwaani mgombea ubunge wa Jimbo la Siha Dk.Godwin Mollel kuzungumza na wananchi wa Sanya juu.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akizungumza katika kampeni za ubunge wa jimbo la Siha.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akiwa na mgombea ubunge wa Jimbo la Siha Dk.Godwin Mollel na viongozi wengine wa CCM.
.........................................................................................

Katibu wa  NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo leo wameuteka mji wa Sanya juu kwa kufanya kampeni za kishindo za ubunge wa jimbo la Siha walipokuwa wakimnadi mgombea kupitia CCM Dk.Godwin Mollel.

Katika kampeni hizo, Viongozi hao wamemnadi mgombea huyo kwa kujikita kwenye hoja za msingi na mipango ya utekelezaji wa ahadi mbalimbali na kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa eneo hilo. 

Akizungumza na wananchi, Dk. Mollel amewaomba wananchi wa Jimbo la Siha kumpa kura za ushindi kwani alipo sasa ndio eneo sahihi la kuwaletea maendeleo ya kweli kwani kwasasa hata zibwa parasta mdomoni wala kulazimishwa kutoka bungeni.


Amewaomba wananchi wa Siha kuungana pamoja kwa maslahi mapanda ya wilaya yao na hatakuwa tayari kuona wananchi wa Siha wanaendelea kukosa uwakilishi makini kwa kuwa awali alilazimishwa kupinga kila kitu na kulazimishwa  kugomea vitu ambavyo vimesababisha kuwakosesha wananchi wa Siha maendeleo ya haraka.

Kutokana na hotuba hizo, Wananchi wa Sanya juu walilipuka kwa shangwe huku wakisema wazi CCM imejaa watu makini na majembe ya uhakika na aina mpinzani kwasasa.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania