CURRENT NEWS

Thursday, January 4, 2018

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AWAANDALIA CHAKULA CHA MCHANA NA KUWAKABIDHI FEDHA WACHEZAJI MABINGWA WA MPIRA UFUKWENI IKULU ZANZIBAR LEO.RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Sand Heroes katika chakula cha mchana alichowaandalia katika viwanja vya Ikulu Zanzibar kwa kuchukua Ubingwa wa Mchezi wa Beach Soka michuano ilioandaliwa na TFF Jijini Da es Salaam baada ya kuingia faina na kuifunga Timu ya Malawi kwa mabao 3 -2.(Picha Ikulu)

WACHEZAJI wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Sand Heroes wakijumuika katika chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuwapongeza na kuwazawadia kila Mchezaji shilingi milioni moja taslim, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar leo.(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa ufukweni Zanzibar Sand Heroes iliotowa Ubingwa wa mchezo huo baada ya kuifunga Timu ya Malawi 3 -2, wakati wa mashindano ya Kimataifa yalioandaliwa na TFF Jijini Dar es Salaam wiki iliopita, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar leo.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimkabidhi mmoja wa Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Sand Heroes shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwapongeza kwa ushindi waliopata wa kulitowa Kombe la Ubingwa wa Mchezo wa Soka la Ufukweli lililoandaliwa na TFF Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwnyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Kombe la Ubingwa wa Mchezo wa Soka la Ufukweni baada ya kukabidhiwa wakati wa hafla ya chakula cha mchana alichowaandaliwa wachezaji hao, akiwa na Waziri wa HabariUtalii Utamaduni na Michezo Zanzibar. Mhe. Rashid Ali Juma.leo Ikulu Zanzibar(Picha na Ikulu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji wa zamani wa Zanzibar na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Znzibar Sand Heroes baada ya hafla ya chakula cha mchana Ikulu Zanzibar leo.(Picha na Ikulu)
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania