CURRENT NEWS

Saturday, January 6, 2018

RC MAHENGE AFUNGA MACHIMBO YA NZUGUNI KUFUATIA MTU MMOJA KUFA MAJI


MKUU wa mkoa wa Dodoma Dk.Binilith Mahenge amefunga na kupiga marufuku shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu zilizokuwa zinafanyika katika eneo la machimbo Nzuguni Manispaa ya Dodoma kufuatia mtu mmoja kufa kwa maji wakati akiwa ndani ya shimo akichimba dhahabu.

Aidha amemwagiza kamishna wa Madini kanda ya kati kushirikiana na uogozi wa Manispaa chini ya Jeshi la polisi kufukia mashimo yote ambayo yalikuwa yanatumika kwa ajili ya uchimbaji wa madini hayo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania