CURRENT NEWS

Sunday, January 28, 2018

UZINDUZI KAMPENI ZA CCM UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE KINONDONI ZAWAVUTIA WENGI.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba (kushoto), akimnadi kwa wananchi mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo viwanja vya Biafra, Dar es Salaam. 
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akiwasalimia wananchi mara baada kutambulishwa na kuitwa jukwaani kumwaga sera zake za kuomba kura wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam . 
Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni Maulid Mtulia akizungumza mambo mbalimbali mbele ya Wanachama wa chama hicho na Wananchi kwa ujumla mara baada kutambulishwa na kuitwa jukwaani kumwaga sera zake za kuomba kura wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam.
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimara Chadema, Ngudu Pascal Manota akiwasalimia wananchi wa Kinondoni jioni ya leo alipokuwa akitambulishwa kwao na kurudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na CCM,pichani kati ni Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba na kulia kwake ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Stephen Wasira
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kimara Chadema, Ngudu Pascal Manota akirudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na CCM,Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akiitazama kadi hiyo kwa makini
Aliyekuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Muslim Hassaanal ambaye hivi karibuni alihamia CCM,akimwombea kura za ushindi Mgombea Ubunge wa jimbo la Kinondoni ,Maulid Mtulia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, Dar es Salaam. 
Mgeni rasmi wa Uzinduzi wa kampeni za chama cha CCM, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mwigulu Nchemba akizungumza mbele ya umati wa watu waliofika kuhudhuria uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi mdogo kwenye viwanja vya Biafra, jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo,katika viwanja vya Biafra Kinondoni jioni ya.
Baadhi ya wananchi na wafuasi wa chama cha CCM wakisikiliza kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye jukwaa la uzinduzi wa kampeni Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Kinondoni,mapema jijini Dar.PICHA NA MICHUZI JR.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania