CURRENT NEWS

Wednesday, January 17, 2018

UZINDUZI WA KUELEKEA SIKU YA MAADHIMISHO YA WANYAMA PORI DUNIANI.
Katibu Tawala wa wilaya ya chemba ndg.nyakia ally akiwataka wananchi wa wilaya ya chemba kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti ,sambamba na kutunza mazingira ya asili ya wanyama pori  na pia katika zoezi hilo jumla ya miti elfu 2000 imepandwa katika kijiji cha Kelema Kuu kata ya Paranga ,maeneo ya taasisi na makazi ya watu


Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya chemba dkt.semistatus  mashimba akitoa shukrani kwa asasi ya kiraia Rafiki Wild Life Foundation pamoja na wakala wa misitu tanzania kwa kuungana kwa pamoja katika zoezi la upandaji miti
Katibu tawala wa wilaya ya chemba ndugu nyakia ally kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya chemba mhe.simon odunda akifanya zoezi la upandaji miti katika kijiji cha kelema kuu ikiwa chemba imechaguliwa kuwa sehemu ya maadhimisho ambapo uzinduzi wa kuelekea siku ya maadhimisho ya wanyama pori duniani kitaifa utafanyika marchi 3/2018 katika mkoa wa dodoma ambapo mgeni rasmi atakuwa waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa tanzania mhe.kassim majaliwa
........................................................................

Na Shani Amanzi,

Uzinduzi wa kuelekea siku ya Maadhimisho ya Wanyama Pori Duniani Kitaifa, utafanyika Marchi 03, 2018 katika Mkoa wa Dodoma ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa na Wilaya ya Chemba imechaguliwa kuwa sehemu ya Uzinduzi wa Maadhimisho hayo kwa shughuli ya upandaji miti iliyofanyika katika kijiji cha Kelema Kuu ,tarehe 15 Januari, 2018.

Katika uzinduzi huo Mgeni Rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Chemba Ndugu. Nyakia Ally kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga.  

Ndugu. Nyakia amesema, Jamii inatakiwa kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti, sambamba  na kutunza mazingira ya asili ya Wanyama Pori. 

Aliongeza kwa kusema zoezi la upandaji miti ni endelevu katika Wilaya ya Chemba na jumla ya miti elfu 2000 imepandwa katika kijiji cha Kelema Kuu kata ya Paranga, maeneo ya Taasisi na Makazi ya watu.

Wilaya ya Chemba imefanya shughuli ya upandaji miti katika Kijiji hicho kama sehemu ya kuunga mkono mkakati wa Serikali wa kuufanya Mkoa wa Dodoma kuwa wa kijani, sambamba na uhamasishaji wa utunzaji wa Wanyama pori kwa kuwa kijiji cha Kelema Kuu kinapakana na pori la akiba la Swagaswaga.

Pori la akiba Swaga swaga linatumika katika shughuli za Uwindaji wa Kitalii ambapo jamii inayozunguka pori hilo inanufaika kwa kupata mgao wa ruzuku unaotokana na shughuli za utalii.

Maadhimisho ya Uzinduzi wa siku ya Wanyama Pori Duniani umeshirikisha Katibu Tawala Wilaya ya Chemba Ndg. Nyakia Ally kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba ,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt. Semistatus H. Mashimba, Mkurugenzi wa Taasisi ya Rafiki Wild Life Foundation, Wakuu wa Idara/Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Viongozi wa Ngazi ya Kata, Kijiji na Wananchi.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania