CURRENT NEWS

Thursday, January 4, 2018

WANANCHI WA WILAYA YA CHEMBA WAHAMASISHWA KUTUMIA FURSA YA KUJIPATIA KIPATO KWA KUTUMIA MIFUGO WALIYONAYOMkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Simon Langoi amewataka Wananchi wa Wilaya ya Chemba kutumia fursa ya kujipatia kipato kwa kutumia mifugo waliyonayo,aliyazungumza hayo mapema leo alipokuwa ofisini kwake Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na kusema changamoto walizokuwa nazo katika Idara yake mwaka  jana ( 2017) ni kutokana  na upungufu wa rasilimali hasa rasilimali watu na upatikanaji hafifu wa chanjo mbalimbali za mifugo(Kichaa cha mbwa,CBPP,CCPP n.k )

    .............................................................

Na Shani Amanzi,

Wananchi wa Wilaya ya Chemba wamehamasishwa kutumia fursa ya mifugo waliyonayo katika kuwapatia kipato na siyo  kwa ajili ya matumizi ya nyumbani  pekee kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na wingi wa mahitaji ya kifedha kwa ajili ya shughuli zao za kimaendeleo.

Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Simon Langoi aliyazungumza hayo mapema leo 04/1/2018 alipokuwa ofisini kwake Halmashauri ya Wilaya ya Chemba na kusema changamoto waliyokuwa nayo ni upungufu wa rasilimali watu na upatikanaji hafifu wa chanjo mbalimbali za mifugo(Kichaa cha mbwa,CBPP,CCPP n.k )
Bw. Simon aliongeza kwa kusema 

“kumekuwepo na mwitikio mdogo wa Wafugaji katika uchanjaji wa Mifugo yao hasa Mbwa (kichaa cha Mbwa) na Kuku dhidi ya Kideri ,Ukosefu wa Malisho na Maji  katika maeneo mbalimbali”.

“Lakini katika maboresho ya mikakati endelevu  ya Idara ya Mifugo na Uvuvi kwa Wananchi  tumepiga hatua kwa  kukinga mifugo dhidi ya magonjwa mbalimbali kama Kichaa cha Mbwa (Rabies) na Kideri kwa Kuku (Newscastle desease) kwa kuwachanja ili kupunguza vifo toka 20% mpaka 10% , kutibu Mifugo  na kutoa tiba kwa Mifugo dhidi ya Magonjwa mbalimbali kama FMD, Minyoo na Magonjwa ya Ngozi”.

Kumekuwepo na migogoro baina ya Wakulima na Wafugaji  juu ya matumizi bora ya ardhi hasa maeneo ya  malisho na kilimo. Halmashauri ya Wilaya ya Chemba kwa kushirikiana na wataalam wa Wizara ya Mifugo,Viongozi wa Serikali za mitaa pamoja na wananchi, imekuwa katika kufanya maamuzi ya pamoja katika kutenga maeneo ya malisho ili kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji.

Wito kwa wafugaji wa Wilaya ya Chemba ni kuhakikisha wanajitokeza kupiga chapa kwa maendeleo ya sekta na pia wanafuga mifugo michache yenye tija na inayoendana na rasilimali zilizopo.

Zoezi la Upigaji Chapa ni endelevu na tayari kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba tumefanya zoezi kwa zaidi ya 103% ya lengo, kuelimisha wafugaji wa mbuzi wa maziwa katika vijiji vya Mondo ,Hamai na Songolo ili kuongeza kipato chao na kuboresha lishe zao huku  mbinu shirikishi (PPP) ikitumika kati ya Halmashauri na Kanisa la KKKT- Arusha kwenye mradi wa Mbuzi  wa Maziwa.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania