CURRENT NEWS

Wednesday, January 3, 2018

WAZIRI JAFO AKERWA HOSPITALI YA WILAYA YA HAI KUSHINDWA KUFUNGA MFUMO WA GoTHoMIS

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwasili katika Hospital ya Wilaya ya Hai kukagua ujenzi wa miundombinu ya Afya.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(kulia)akikagua ujenzi wa Duka la Dawa linaloendelea kujengwa katika Hospital ya Wilaya ya Hai.
Hii ndiyo Hospital ya Wilaya ya Hai ambayo mpaka sasa haijafunga mfumo wa Uendeshaji na Usimamizi wa  Kutolea huduma za Afya -   GoTHoMIS.

    .........................................................

Nteghenjwa Hosseah,Hai.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amekasirishwa na uongozi wa hospital ya Wilaya ya Hai kwankushindwa kutumia mfumo wa Uendeshaji na Usimamizi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya (GoTHoMIS).

Waziri Jafo akiwa ziarani Katika Wilaya hiyo kukagua ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Hospital ya Wilaya alihoji endapo Hospital hiyo imeanza kutumia mfumo wa  GoTHoMIS katika uendreshaji na usimamizi wa huduma za Afya ikiwa ni agizo alilolitoa miezi michache iliyopita wakati alipotembelea Hospital hiyo.

Majibu aliyoyapata katika Hospital hiyo hayakumridhisha ambapo Uongozi wa Hospital na Wilaya hiyo ulidai kutokua na mtaalam wa mifumo  ya Tehama wa kusimamia usimikaji wa Mfumo  ilihali vifaa vyote kama vile Computer kwa ajili ya matumizi ya mfumo vimekwishafika tayari kuanza kutumika.

“Haiwezekani Halmashauri za pembezoni watumie mfumo huu katika uendeshaji wa shughuli zao na nyie wa Mjini kabisa mpaka leo mnasingizia eti hamna mtaalamu,  mlishindwa kutafuta hata kutoka katika Halmashauri za Jirani  au mna vitu mnavifanya na mnaona mfumo ukianza kutumika hamtaweza kuendelea kufanya tena hayo mnayoyaficha ”

Aliongeza kuwa mapato mnayokusanya katika Hospital hii hayaridhishi ukilinganisha na Idadi ya wagonjwa wanaokuja kutibiwa kwa siku na mkianza kutumia Mfumo huu utaonyesha mapato sahihi ambayo mnakusanya na hili ndio ninaloona mnalikwepa, sasa ninawapa wiki mbili tu mfumo huu uwe umeanza kutumika.

 Akitoa Taarifa ya Hospital hiyo mganga Mkuu wa Wilaya hiyo alisema mapato yanayokusanywa kwa mwezi ni zaidi ya Mil. 50 na kwa kipindi cha Miaka 50 wamekusanya zaidi ya Mil 300 na baada ya kukamilisha ujenzi wa Duka la Dawa la Hospital hiyo watakusanya Fedha nyingi Zaidi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai amemuahidi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo kuwa mfumo huo utakamilika ndani ya wiki moja na utaanza kutumika katika kusimamia na kuendesha shughuli za utoaji wa huduma za Afya katika Hospital ya Wilaya ya Hai.

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania