CURRENT NEWS

Thursday, January 4, 2018

WAZIRI JAFO AKWAZWA NA UBOVU WA BARABARA YA MNYAMANI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akikagua barabara na Mnyamani-Vingunguti wakati wa ziara yake katika Manispaa ya Ilala.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akitoa maelekezo kwa Viongozi wa Manispaa ya Ilala wakati wa ukaguzi wa barabara ya Mnyamani-Vingunguti.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(katikati) akiwa na Mbunge wa Segerea Mhe.Bonna Kaluwa wakati wa ukaguzi wa barabara ya Mnyamani-Kaluwa.

    ......................................................

Nteghenjwa Hosseah, Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selamani Jafo amekerwa na ubovu wa miundombinu ya barabara ya Mnyamani-buguruni inayosababisha adha kwa wananchi wa maeneo hayo na kukwamisha shughuli zao za maendeleo za wananchi hao.

Waziri Jafo ameonyesha hali hiyo wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kukagua barabara ya Mnyamani na Kituo cha Afya Buguruni kuangalia ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi wa maeneo hayo na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

“Haiwezekani barabaraba hii iharibike kwa kiasi hiki lakini Viongozi wa Manispaa hii mpo na mnaendelea na kazi Ofisini, wananchi wanateseka, magari yao yanaharibika, vyombo vingine haviwezi kupita katika barabara kutokana na ubovu wa barabara hii ila nyie  hamuoni matatizo haya ya wananchi, mmekaa tu Ofisini wala hamtafuti suluhisho la haraka la kutatua vhangamoto hii” Alisema Jafo.

Aliongeza kuwa ninatoa wiki moja kwa Uongozi wa Manispaa ya Ilala, Tatura Wilaya na Mkoa pamoja na Shirika la Maji linalotoa huduma katika Mkoa wa Dar es Salaam(Dawasco) kukutana na kukubaliana kwa haraka Suluhisho la kudumu na kuanza kuitekeleza na ili kumaliza changamoto hii kwa wananchi wa Buguruni.

“Kwa ubovu ninaoushuhudia katika barabara hii sitapenda muanze kujivuta sijui vikao visivyoisha, majadiliano ya muda mrefu mimi ninatoa Wiki moja tu kazi iwe imeanza na Tar 12/01/2017 nitakuja tena kukagua na kuona maendeleo ya ukarabati wa barabara hii na endapo kazi itakua haijaanza ntashughulika na Viongozi wa Ilala” Alimalizia Waziri Jafo.

Akiwasilisha kero za wananchi wake mbele ya Waziri Jafo Mbunge wa Segerea Mhe.Bonna Kaluwa amesema Maeneo ya Mnyamani na Vingunguti yana wakazi wengi sana ambao wengi wao hujishughulisha na biashara katika maeneo hayo.

Mhe.Bona aliongeza kuwa ubovu wa barabara ya kwa Mnyamani imesabisha wananchi wa maeneo hayo kufunga biashara zao kwa sababu wakati wa mvua hakuna mteja anayeweza kufika kwenye biashara, wengine wamehama makazi yao kwa sababu ya maji yaliyojaa kwenye mashimo makubwa yaliyopo kwenye barabara hiyo hii ni adha kubwa kwetu tunaomba Serikali itusaide.

Akitoa maelezo ya ubovu wa barabara hiyo Meneja wa Tarura Wilaya ya Ilala amesema ubovu wa barabara hiyo unachangiwa na  ubovu wa miundombinu ya Maji iliyoko chini ya Dawasco ambayo kila mara bomba linalopita katika eneo hilo hupasuka na kumwaga maji mengi yanayopelekea kubomoka kwa Lami iliyowekwa na kwa sababu barabara hiyo inatumiwa na magari mengi hupelekea kuwa na mashimo makubwa kama haya yanayoonekana hivi sasa.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania