CURRENT NEWS

Friday, January 26, 2018

WAZIRI JAFO ATAKA TSC KUHARAKISHA KUPANDISHA MADARAJA WALIMU.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani
Jafo akifungua Mkutano wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa
Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.

 Katibu wa Tume ya Walimu (kushoto aliyesimama) Mwl. Winifrida G. Rutaindurwa
akiwasilisha taarifa ya Tume katika Mkutano wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za
Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu Bw.Oliva Paul Mhaiki akitoa neon la
utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa wa Kazi wa
Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha
Mipango,Mjini Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe wakifuatilia Mkutano wa wa Kazi wa Wajumbe wa Kamati za
Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha Mipango,Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani
Jafo(Aliyekaa katikati) katika Picha ya Pamoja na Sekretariet ya Mkutano wa Kazi wa
Wajumbe wa Kamati za Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika katika chuo cha
Mipango,Mjini Dodoma.

           ................................................................................................................

Nteghenjwa Hosseah, TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Selemani
Jafo ameitaka Tume ya Utumishi wa Walimu(TSC) kusimamia na kuhakikisha
Walimu wote wanapanda madaraja kwa wakati na kwa mujibu wa Elimu zao ili
kupunguza Malalamiko ya Walimu wetu Nchini.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wajumbe
wa Kamati ya Tume za Utumishi wa Walimu za Wilaya kwa Mikoa ya Dodoma,
Morogoro na Singida uliofanyika katika Chuo cha Mipango ya Maendeleo
Vijijini kilichopo Mkoani Dodoma mapema leo Tarehe 26/01/2017.

Waziri Jafo alisema kuwa kumekuwa na malalamiko, manunguniko na
masononeko ya muda mrefu toka kwa Walimu kuhusu suala hili ya Upandaji
wa madaraja halifuati taratibu aliyeajiriwa mwaka 2000 na anaweza kuwa
sawa na yule aliyeajiriwa mwaka 2008 na wengine wamejiendeleza Kielimi
lakin hakuna mabadiliko yoyote madaraja yao.

‘Tume hii ifanye kazi ya kurudisha hadhi ya Walimu, iwajengee heshima na
thamani yao katika Jamii, shughulikieni malalamiko yao ya Msingi madaraja
yao yapande kwa kuzingatia muda waliokaa kazini, elimu yao na Utendaji wao
wa kazi; Hilo lisitegemee “favour” ya Katibu wa Watumishi wa Tume waliopo
katika eneo husika’

Wakati huo huo, Waziri Jafo alisisitiza  wajumbe wa Kamati za Tume ya
Utumishi wa Walimu kuwa Mkutano huu utumike kupeana maarifa ya kazi,
jinsi gani mnaweza kufanya kazi kwa Usahihi zaidi kwa kuzingatia Sheria
iliyounda TUME YA UTUMISHI WA WALIMU ya mwaka 2015 na Kanuni zake za
mwaka 2016.

‘Tume hii Ndio iwe Kimbilio la Walimu, iwe tegemeo la Utatuzi wa matatizo
yote ya Walimu kwa sababu Tume ya Walimu ndio muajiri wa Walimu,
Inasimamia Nidhamu za Walimu na mchakato mzima unaohusi Ajira za
Mwalimu awapo kazini hivyo mfanye kazi kwa Haki, mkaepuke rushwa, Mkawe
na busara na Hekima katika kutatua changamoto za Walimu’ 

Aidha Waziri Jafo hakusita kuwakumbusha wajumbe wa Tume ya Utumishi wa
walimu kuhusu mgawanyo wa Walimu katika halmashauri kwa kuzingatia
vipindi wanavyotakiwa kufundisha na uwekaji wa takwimu sahihi za Walimu
waliopo sasa, wanaotarajiwa kustaafu kwa mwaka huu na kuweka maoteo ya
ajira mpya zitakazohitajika kutokana na nafasi zitakazoachwa na wale
wanaostaafu hivi karibuni.

“Takwimu zisiwe za kubahatisha tena kupitia Tume hii mhakikishe mnakuwa na
Takwimu sahihi kwanza za mgawanyo wa Walimu katika kila Halmashauri je
mgawanyo wa walimu waliopo Malinyi ni sawa na mgawanyo wa Walimu
waliopo Manispaa sio Mwalimu wa Manispaa anafundisha vipindi viwili kwa
wiki wakati anatakiwa kufundisha 20 na pia mahitaji ya walimu kulingana na
masomo wanayofundisha maoteo kwa kuzingatia idadi ya wale wanaostaafu”
Alisema Jafo.

Aidha Jafo alitaka ifanyike tathmini ya kina uhusu maadili ya walimu na wanafunzi na kwa walimu wanaovunja Sheria, Kanuni na maadili ya kazi ya waalimu ikiwemo uzembe , utoro kazini, rushwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Naye, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu Ndg.Oliva Mhaiki alisema
wajumbe wa kamati za TSC Wilaya waliteuliwa rasmi na Tume katika mkutano wa
Tar 20-25/02/2017 na tangu walipoteuliwa na kuanza kutekeleza majukumu yao
hawakuwahi kupewa mafunzo yeyeote hivyo Sekretariet imeona upo umuhimu wa
kufanya mkutano wa kazi kwa lengo la kuelekezana wajibu na majukumu yao kama

kamati.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania