CURRENT NEWS

Monday, February 5, 2018

CCM YATOA DOZI KALI KWA CHADEMA KATA YA MANZASE.

 Naibu katibu mkuu wa CCM bara ndugu Rodrick Mpogolo akionyesha kadi aliyokabidhiwa na aliyekuwa mgombea wa Chadema Mashaka Chalo,kushoto kwake ni Chalo aliyerudi CCM,mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Godwin Mkanwa na mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde.
 Naibu katibu mkuu wa CCM bara ndugu Rodrick Mpogolo akizindua kampeni za uchaguzi mdogo kata ya Manzase mjini Dodoma.
 Baadhi ya wananchi na wanachama wa Kata ya Manzase waliohudhuria uzinduzi wa kampeni katika kata hiyo.
 Baadhi ya wabunge walioshiriki uzinduzi wa kampeni wa Kata ya Manzase wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Naibu katibu mkuu wa CCM Bara ndugu Rodrick Mpogolo akimnadi mgombea wa udiwani kata ya Manzase kwa yiketi ya Chama hicho Amos Mloha katika uzinduzi wa kampeni katika kata hiyo.

...................................................................................................................
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Bara ndugu Rodrick Mpogolo amezindua kampeni za uchaguzi mdogo katika Kata ya Manzase iliyopo wilayani Chamwino mkoani Dodoma huku akipewa zawadi ya kumpokea na kumkabidhi kadi aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)Mashaka Chalo.

Chalo alikuwa mgombea wa Chadema na juzi alinadiwa na baadhi ya wabunge wa Chama hicho katika ufunguzi wa kampeni ili apeperushe bendera yao katika uchaguzi huo lakini sasa amejiunga na CCM.

Mbali na Chalo  wanachama wengine 129 wa CHADEMA akiwemo mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la chama hicho BAWACHA wilaya ya Chamwino Ruth Mpali nao wamekihama chama hicho na kuhamia CCM.

Akimkabidhi kadi mwanachama huyo Mpogolo amemkaribisha katika chama na kusema zawadi aliyoipata ni muendelezo wa kazi nzuri inayofanywa na rais John Magufuli.

“Nimeona mtikisiko wa madiwani na wabunge wakitaka kuja CCM,chama hiki kinapendwa,chama hiki ni kikubwa na kinaheshimika tunawakaribisha sana mjisikie mpo nyumbani,moja ya vigezo vya chama kupendwa na kukubalika ni uchaguzi ambao matokeo ya uchaguzi huo CCM imekuwa ikishinda kwa kishindo,”alisema Mpogolo.

Akimnadi mgombea wa udiwani katika kata hiyo ndugu Mpogolo amewataka wana Manzase kumchagua Amos Mloha kuwa diwani wa kata hiyo.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mtera ambalo Kata ya Manzase ipo ndani yake Livingstone Lusinde amesema hiyo ni dawa kwa vyama ambavyo haviandai wagombea kama Chadema.

“Tarehe 10 mwezi huu Chadema walikuja Manzase kumtafuta mgombea walikuja kwa Elias,ambaye alikataa wakaja kwa Mashaka,kabla ya Mashaka kujibu chochote  akanipigia simu nikamwambia kubali wakaingia mkenge wakamezeshwa ndoano na hii maana yake game limekwisha,

"Hii safari hii kiboko,tumezoea kupokea madiwani na wabunge wakihama chama na kujiunga na CCM lakini leo hapa ni mgombea ndio ameondoka,Chadema jitafakarini,”alisema Lusinde.

Uzinduzi huo pia ulihudhuriwa na wabunge wa viti maalum Angelina Malembeka,Mariam Ditopile,Fatma Tawfiq,Felister Bura na mbunge Korogwe Vijijini Steven Ngonyani(Majimarefu).
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania