CURRENT NEWS

Thursday, February 15, 2018

E-PASSPORT: WALIOTOSWA KUTAFUNA BILIONI 400 WAHAHA

Na Ibrahim Malinda. Mambo mazito yameibuka yakilihisisha gazeti moja la kila wiki kuhongwa mamilioni ya pesa ili kuichafua serikali wakiituhumu kwa tuhuma za uongo kuhusiana na mradi wa hati za kusafiria na uhamiaji kwa ujumla. Hivi karibuni Gazeti hili liliripoti kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, alizindua rasmi mfumo mpya wa upatikanaji wa hati za kusafiria katika hafla iliyofanyika makao makuu mwa jeshi la uhamiaji kurasini jijini Dar es Salaam huku akiibua siri ya kutaka kutafunwa kwa mabilioni ya shilingi katika mchakato wa utekelezaji wa mradi huo. 
 Katika hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa pia na viongozi mbalimbali wa kitaifa na viongozi wastaafu, Rais pia alitumia hadhira hiyo kulipongeza jeshi hilo la uhamiaji kwa maboresho makubwa hasa kwenye Nyanja ambazo hapo awali palikuwa na mapungufu makubwa yaliyopelekea idara hiyo muhimu kuonekana kupoteza heshima mbele ya jamii ya ndani na ile ya kimataifa kiasi cha kupelekea kushindwa kukamata wahamiaji haramu, kushindwa kudhibiti hati za kusafiria mpaka kumilikiwa na watu wasio watanzania, kuichafua hati ya kusafiria kiasi cha kupelekea watanzania kusimamishwa na kucheleweshwa ikibidi kuzuiwa kuingia pindi wasafiripo kwenda nchi nyingine sambamba na vitendo vya rushwa iliyoonekana kukithiri katika idara hiyo siku za awali.
 ‘’Unakuta muhamiaji haramu amesafiri kutoka huko akapita chato, kagera, mwanza mpaka anakuja kukamatiwa Singida, utafikiri huko alikopita hakukuwa na maafisa wa uhamiaji, kamishna tafadhali akikamatwa mtu wa aina hii, shughulikia nidhamu ya wakuu wa uhamiaji wa mikoa alipopita mtu hiyo ikibidi hata kuwapunguzia vyeo na nyota zao’’. Alisema Rais Magufuli 
 Rais aliongeza kuwa hati za kusafiria ni kitu muhimu sana kwa nchi yoyote ile na kile mwenye haki ya kuipata anatakiwa kufuata wajibu wake kuhakikisha anaipata ili imuwezeshe kusafiri nje ya nchi na kwamba hati hizi za kisasa zitakuwa zinapatikana kwa gharama ya shilingi laki moja na elfu hamsini tu (150,000/=) gharama ambayo inaonekana ni nafuu kulinganisha na hadhi, uimara ubora na matumizi wa hati hizo na kulinganisha na gharama zinazotozwa katika nchi nyingine zilizoanza kutumia mfumo huo. 
 Akiendelea kuhutubia katika uzinduzi huo Rais amesema kuwa awali wajanja walipanga kuutekeleza mradi huo kwa gharama kubwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 226 ambazo ukizibadili kwa Dola moja sawa na shilingi 2245 mradi huo ungegharimu shilingi za kitanzania bilioni 507 na kwamba baada ya kugundua ujanja huo Rais alivituma vyombo vya dola kufuatilia na kubainika kuwa mradi huo unaweza kutekelezeka kwa gharama nafuu na za kawaida ambapo baadae mradi umeonyesha kutelekezwa kwa dola milioni 57.8 sawa na bilioni 129 za kitanzania na hivyo kuliokolea taifa upotevu ambao ungeweza kujitokeza wa zaidi ya shilingi bilioni 380. 
 Katika hafla hiyo Rais amemuahidi kamishna mkuu wa uhamiaji nchini Kamishna Anna Peter Makakala kuwa atawapatia idara hiyo shilingi bilioni kumi ili ziwasaidie kurahisha ujenzi wa ofisi yao ya makao makuu mjini Dodoma ofisi ambayo itakuwa na hadhi sawia na idara yenyewe husika. 
 Aidha Rais Magufuli amewakumbusha watumishi wa idara hiyo kuzingatia weledi, kutokuendekeza rushwa kuwa wazalendo na kuwajiika ili kuhakikisha wanawahudumia watanzania huku wakiendelea kukusanya mapato yatokanayo na huduma wazitoazo na akaonyesha kushangazwa iwapo mapato hayata ongezeka baada ya kuanza kutekelezwa kwa mradi huo. 
 Miongoni mwa vitu vilivyomfurahisha Rais Magufuli kwenye utendaji kazi wa idara hiyo muhimu nchini ni pamoja na kuanza kwa ukusanyaji mapato kwa mfumo wa kielektroniki katika makao makuu ya idara hiyo ya Dar es Salaam,mfumo mpya kuhakiki vibali vya ukaaji na kuhamia Dodoma kutekeleza uamuzi wa Serikali kwa vitendo Taarifa za uhakika zilizonaswa na gazeti hili zinasema kuwa mmoja kati ya mawaziri waandamizi wa serikali iliyopita ndiye aliyeileta kampuni ya kiingereza ya De ra Lue kampuni ambayo ilitaka kupiga dili hilo la kuandaa hati kwa bilioni 500.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania