CURRENT NEWS

Saturday, February 17, 2018

JAFO AAGIZA KUKAMILISHWA KWA MRADI WA MAJI KILUVYA

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Makurunge katika kata ya Kiluvya wilaya ya Kisarawe.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa michezo wa shule ya Msingi Kiluvya B.

 Wanafunzi wa Shule ya msingi Mlonganzila wakimpokea kwa shangwe Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo.
Wananchi wa Kiluvya B wakiwa katika mkutano walipotembelewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo.
  ...............................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo amewaagiza wataalam wa maji wilayani Kisarawe kumsimamia mkandarasi wa mradi wa maji wa Kiluvya- Makurunge kukamilisha mradi huo kwa kuondoa dosari ndogo ndogo zilizopo ili wananchi waweze kupata maji ya uhakika.

Jafo ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kuongea na wananchi na ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Katika ziara yake, Jafo amefanikiwa kutembelea maeneo ya Makurunge, Kiluvya na Mloganzila ambapo amekagua miradi ya elimu, afya na maji.

Akiwa katika mradi huo wa maji, Waziri Jafo amesema pamoja na Mradi huo kukamilika lakini kuna dosari ndogondogo ambazo zinapaswa kushughulikiwa ili maji yaweze kupatikana muda wote kwa wananchi.

Aidha Jafo amewaagiza wataalam kutembelea maeneo yao ya kazi ili kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazojitokeza hususan huduma za vyoo, maji, na uchakavu wa miundombinu.

Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amechangia mifumo ya saruji 450 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi Kiluvya A na kuanza ujenzi wa sekondari ya Mloganzila.

Aidha ameelekeza upelekwaji wa fedha za ujenzi wa  vyumba viwili vya  madarasa katika shule ya msingi Mloganzila ambapo ujenzi huo unatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki ijayo.


 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania