CURRENT NEWS

Saturday, February 10, 2018

JAFO AAGIZA TATHMINI YA KINA IFANYIKE KUKAMILISHA JENGO LA HALMASHAURI YA CHAMWINO.

  
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akitoa maagizo kwenye ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.


 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Chamwino Vumilia Nyamonga wakati akitoa maelezo kuhusu eneo lililotengwa kwa ajili ya uboreshaji Kituo cha Afya Chamwino.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akizungumza mara baada ya kujionea eneo litakalotumika kuongeza majengo ya Kituo cha Afya Chamwino.

    ...................................................................

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na kuagiza Wakala wa Majengo(TBA)na Suma JKT kuangalia njia bora ya kulifanya jengo hilo liweze kukamilika kwenye ubora unaotakiwa ili watumishi wahamie.

Watumishi wa Halmashauri hiyo kwasasa wanatumia jengo la Mkuu wa wilaya hiyo kutokana na jengo lao kutokamilika.

Jafo ametoa kauli hiyo leo alipotembelea kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa mwezi Novemba mwaka jana, ambapo aliagiza ujenzi huo ukamilike ifikapo Januari mosi mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kukagua ujenzi huo, Jafo amesema ameridhishwa na sababu zilizotolewa zilizofanya kukwama kukamilishwa kwa jengo hilo.

Amesema sababu zilizotolewa ambazo mkandarasi amekumbana nazo ameona ni vyema watumishi wakaendelea kuvumilia kutumia ofisi ya Mkuu wa wilaya hadi hapo itakapokamilika kwenye ubora unaotakiwa.

Waziri Jafo amewataka kuifanya tathmini hiyo na kwamba kwa kuwa wanaelekea katika mipango ya bajeti wataangalia namna ya kushirikiana na Halmashauri ili jengo liweze kukamilika.

Awali, Mkandarasi kutoka Suma JKT, Mhandisi David Pallangyo amesema ukamilishaji umekwamishwa kutokana na hali ya hewa na pia makosa yaliyofanywa na mkandarasi wa awali.

“Hapa hii flow ya chini tuliona tuikamilishe lakini hali ya hewa na hizi mvua maji yanajaa hivyo tunafanya tathmini kama tutaweza ni vyema tukaweka water proof,”amesema

Aidha Mkandarasi Mshauri kutoka TBA, Mhandisi Vilumba Sanga amesema wanafanya tathmini katika jengo hilo kuangalia namna ya kulikamilisha kwa kushirikiana na Suma JKT.

“Tunafanya ‘estimate’ ya water proof maana maji yanajaa, hii inatokana na makosa yaliyofanywa na mkandarasi wa awali, huyu mkandarasi wa sasa anakutana nayo site,”amesema Sanga

Katika hatua nyingine, Waziri Jafo ametembelea Kituo Cha Afya cha Chamwino Ikulu kuangalia uboreshaji wa kituo hicho ambacho kimeingiziwa Sh.Milioni 500 kwa ajili ya kujenga Wodi ya akina mama na watoto, maabara, Chumba cha Kuhifadhia maiti.


Hata hivyo, amekuta ujenzi huo haujaanza kutokana na eneo linalotakiwa kujengwa kuwa dogo na hivyo kuahidi kufanya tathmini halisi kwa kushirikiana na wataalam kuangalia uwezekano wa kujengwa jengo la ghorofa.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania