CURRENT NEWS

Wednesday, February 21, 2018

JAFO AHAMASISHA WADAU WA ELIMU

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akipokea madawati 70 kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na dawa(TFDA).
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na Mbunge wa Mvomero Suleiman Saddiq na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk.Steven Kebwe.
 Viongozi wakikagua madawati yaliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa(TFDA).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na viongozi wengine wa mkoa wa Morogoro.
 .............................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,TAMISEMI Selemani Jafo amewataka wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu  bora.

Jafo ameyasema hayo wakati akipokea msaada wa madawati 70 kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa(TFDA) kwa ajili ya shule za Halmashauri ya wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.  

Jafo amewaomba wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi za serikali na Taasisi binafsi kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Magufuli anazozifanya katika sekta ya elimu ambapo takriban sh. bilioni 23 hutolewa kila mwezi kwa ajili ya kugharamia elimu bila malipo. 

Kwa upande wake, Mbunge wa Mvomero Suleiman Saddiq ameiomba serikali na wadau kuendelea kuzisaidia shule za Mvomero kwa upande wa madawati na vyumba vya madarasa.

Amesema programu ya elimu bila malipo imesababisha wazazi wengi kuwapeleka watoto wao shuleni hivyo kusababisha madawati na vyumba vya madarasa kuwa ni changamoto kubwa wilayani humo.


Pia amempongeza Waziri Jafo katika jitihada zake za kuwahudumia watanzania.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania