CURRENT NEWS

Sunday, February 18, 2018

JAFO ASIFU UJENZI WA MIRADI KWA ‘FORCE ACCOUNT’

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na wananchi wa Mitengwe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madarasa mapya.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jafo akizindua mradi wa madarasa uliowezeshwa na serikali kwa kushirikiana na wananchi.
 Madarasa mapya ya Shule ya msingi Mitengwe yaliyozinduliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo.
 Wananchi wa kijiji cha Mitengwe wakiwa katika mkutano wa hadhara wakati wa ufunguzi wa madarasa mapya.
Katibu Tawala wa wilaya ya Kisarawe Mtera Mwampamba akielezea jinsi wananchi walivyoshiriki katika ujenzi wa madarasa.
.......................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo amesifu miradi inayojengwa kwa utaratibu wa ‘Force Account’ kwa kuwa imekuwa na ubora wa hali ya juu kwa thamani ndogo huku utekelezaji wake ukishirikisha wanajamii wenyewe.

Jafo ameyasema hayo leo alipokwenda kuzindua mradi wa madarasa manne, Ofisi ya walimu, pamoja na matundu 10 ya vyoo katika shule ya msingi Mitengwe wilayani Kisarawe mkoani Pwani. 

Amesema ujenzi huo umetumia utaratibu wa ‘Force Account’ na imejengwa kwa ubora na kwa thamani ndogo.

Katika uzinduzi huo, Waziri Jafo amesema kwamba amezunguka katika Halmashauri mbalimbali hapa nchini kukagua miradi ya vituo vya afya na miradi ya elimu inayogharamiwa na serikali imejengwa vizuri.

Amewashukuru watanzania wote kwa kuunga mkono juhudi za serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kushiriki kwa pamoja katika kujenga miundombinu hiyo.


Akiwa katika mkutano wa hadhara, kijiji cha Mitengwe, Jafo amesema Rais Magufuli na serikali yake ameamua kuibadilisha nchi kwa kuboresha huduma za jamii ili kuwaondolea kero wananchi na kuharakisha maendeleo ya nchi.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania