CURRENT NEWS

Monday, February 12, 2018

KAKUNDA AMSIMAMISHA MHANDISI WA MAJI CHEMBA

 NaibU Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Joseph Kakunda akikagua mradi wa maji Lahoda-Kisanda wakati wa ziara yake Wilayani Chemba.
 Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe.Joseph kakunda (kulia) akizungumza na mwanafunzi Fatuma Ramadhani wakati alipotembelea shule ya Msingi Lahoda.
 NaibU Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Joseph Kakunda akikagua mradi wa maji Lahoda-Kisanda.
Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Joseph Kakunda akizungumza na wananchi wa vijiji vya Lahoda,Kisanda na Honta wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Chemba.
..................................................................
Nteghenjwa Hosseah,Chemba.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais- TAMISEMI Mhe. Joseph George Kakunda ameiagiza halmashauri ya Wilaya ya Chemba kumsimamisha Mhandisi wa Maji wa Halmashauri hiyo kwa kushindwa kusimamia miradi ya maji.

Mhe.Kakunda alitoa maagizo hayo wakati wa ziara yake Wilayani humo aliyoifanya ambapo alikagua miradi ya maji na kuzungumza na wananchi wa vijiji vya Lahoda,Kisande na Honta.

Baada ya kufanya ukaguzi huo na kubaini mapungufu yaliyopo kwenye miradi ya maji sambamba na kumsimamisha Mhandisi wa Maji pia aliagiza OR-TAMISEMI kufanya Ukaguzi wa Kitaalamu (Technical Audit) ya miradi yote ya maji ambayo imeonekana kwa macho kutotekelezwa kwa kiwango na bado
haijaanza kufanya kazi katika Halmashauri ya Chemba.

“Serikali imetoa Fedha nyingi sana kwa ajili ya miradi hii ili kupunguza kero kwa wananchi wetu lakini wasimamizi wa Miradi hawatekelezi wajibu wao ipasavyo katika kusimamia miradi hiyo na wananchi wetu bado wananednelea kuteseka kwa sababu ya Uzembe wa watu wacheche hii haitakubalika lazima wachukuliwe hatua” Alisema Kakunda.


Naibu Waziri Kakunda wakati wa ziara hiyo pia alitembelea Shule ya Msingi Lahoda na alikutana na mwananfunzi mwenye ulemavu wa ngozi na kuelekeza Halmashauri ya Chemba iwe inampatia mahitaji muhimu mwanafunzi huyo.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania