CURRENT NEWS

Saturday, February 17, 2018

MAKAMU MWENYEKITI UVCCM TAIFA ALIA NA UZALENDO

Makamu Mwenyekiti Umoja wa Vijana CCM, Bi Tabia Mwita amewataka vijana kuwa wazalendo na kuwajibika katika mambo chanya yatakayozalisha maendeleo kwa Taifa.


Aidha alisema kuwa ni wakati wa Vijana kuziishi fikra za waasisi wa Taifa na kumsaidia Rais Dkt Magufuli kuyafikia malengo ya Tanzania ya Viwanda ifikapo mwaka 2025.Mwita ameyazungumza hayo leo katika uzinduzi wa Kitabu cha 'Nuru ya Taifa' uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam."Vijana yatupasa tuwe wazalendo na kuthamini yale yanayofanywa na Rais Dokta Magufuli, tujifunze kupitia kitabu hiki kwakuwa kimeeleza kwa kina juhudi za Rais wetu", alisema Mwita.Aidha amemuomba Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dokta Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa vijana ili kutengeneza hazina ya Taifa."Natambua kuwa Waziri wangu unamajukumu mengi ya Taifa, naomba usituchoke vijana wako pale tunapokuja kuomba ushirikiano wako katika masuala yetu ya kimaendeleo kwakuwa ninyi ndio wazee wa nchi yetu" aliongeza Mwita.Pamoja na hayo Mwita amempongeza mwandishi wa kitabu hicho ndugu Gadiell Lameck, ambapo kinaelezea kazi zilizofanywa na Rais Magufuli kwa muda wa miaka 2.
 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania