CURRENT NEWS

Saturday, February 10, 2018

MAKAMU WA RAIS APONGEZA KIWANDA CHA IVORY FOOD& BEVARAGE IRINGA

Makamu wa  Rais  Samia  Suluhu  Hassan  akitembelea  kiwanda  cha Ivori Food & Bevarage leo 

Makamu  wa  Rais  Samia  Suluhu Hassan  katikati  akiongozana na  mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza kushoto na mkurugenzi wa  kiwanda  cha Ivori Food & Bevaragena mkurugenzi Mtendaji Suhail Esmail Thakore


Mkuu  wa   mkoa wa Iringa  Amina Masenza akisalimiana  makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan  leo 
mkurugenzi Mtendaji wa  kiwanda   cha  Ivory Bw Suhail Esmail Thakore akitoa  taarifa ya  kiwanda  hicho 

 Makamu  wa  Rais  Samia Suluhu  Hassan  akizungumza  baada ya  kutembelea  kiwanda  cha Ivory  Iringa 

Na  Matukiodaima Blog 


MAKAMU  wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaSamia Suluhu Hassan  amepongeza  uwekezaji  mkubwa  uliofanywa na kiwanda cha Ivori Food & Bevarage cha Iringa kuwa  ni  hatua  kubwa  ya  mapinduzi  ya  serikali ya viwanda  nchini .

Akizungumza   leo  baada ya  kutembelea   kiwanda   hicho  eneo la  Ipogolo makamu  wa  Rais  alisema  kuwa   serikali imejikita  kuweka  mazingira  bora kwa  wawekezaji  pamoja  na  kuona  wananchi  wanapata  ajira  katika  viwanda   hivyo .

  Ndugu  zangu  tunaelekea  kwenye  Tanzania  ya  viwanda  kwa  kujenga  uchumi  mpya  katika  nchi   yetu kama  tukiwa na  viwanda vitano ama  kumi kama   hivi  basi  uchumi  wetu  utazidi  kukuwa  zaidi “

Hata   hivyo alitaka  ili  kuwa na uchumi  zaidi na  viwanda  kuweza  kusonga mbele  ni  vema  kila mwananchi  kutunza amani  na  kuepuka  kuvuruga amani iliyopo .
  Ninachowaomba  ndugu  zangu  tuchape kazi  Tanzania  yetu  isonge  mbele  hivyo  wote  ambao  mmepata  kazi katika  kiwanda   hiki  chapeni kazi  ili  nchi   yetu   izidi  kuendelea  kiuchumi “

Alisema   kuwa  kiwanda  hicho  kimekuwa  nguzo  kubwa ya  uchumi  katika  mkoa  wa  Iringa na  Tanzania  kwani  ni  miongoni mwa  viwanda  ambavyo  vinafanya   vizuri  na  vinazidi  kujitanua  zaidi kwa  kufunga  mashine  mpya  za  kisasa .

Akitoa  taarifa  ya  kiwanda  hicho  cha Ivori Food & Bevarage na mkurugenzi Mtendaji Suhail Esmail Thakore  alisema  kuwa  kiwanda  kilianzishwa  mwaka 2007  na  kuwa  kiwanda   hicho  kinajishughulisha  na  uzalishaji  mbali mbali  zikiwemo  pipi ,Cocoa Poda, Tomato  Sauce  na  Chocolate .

  Kuwa  kiwqanda   hicho  wakati  kinaanzishwa  kilikuwa na  wafanyakazi 20  na  kilianza  na mtaji  wa  fedha  kiasi cha  shilingi milioni 70   kikiwa  kinazalisha  Tomato Sauce .
  Upanuzi  wa  kiwanda    ulianza mwaka  2009  tulifanya  upanuzi  wa  kiwanda   kwa  kuanzisha  uzalishaji wa  pipi  Ivory  kwa  mtaji  wa  shilingi  bilioni 1.5 mwaka  2014  tulianzisha   kiwanda cha  Chocolate  na  cocoa  Poda kwa mtaji  wa  shilingi  bilioni 3”
 Alisema  kuwa  kiwanda   kinatumia  malighafi   toka  ndani  ya  nchi  ikiwemo cocoa  tpoka  Kyela ,nyanya  toka  Ilula wilaya ya  Kilolo  na mahindi  toka  Iringa  , Ruvuma  na  Rukwa .

Hata   hivyo  alisema  kutokana na  uzalishaji  mzuri  na ubora  wa  bidhaa za   kiwanda  hicho wamefanikiwa  kushindana  na  masoko  ya  nje  kama  Kenya na  nchi  nyingine  hasa  katika  soko la  Pipi na  cocoa Poda .
Tulipo  anzisha  kiwanda  cha  pipi  tulikuwa na  viwanda  saba   katika  soko la Tanzania  hadi   sasa   viwanda    vilivyobaki  ni  viwili  na  tuna  mshindani   aliyebaki  ambaye  ana hali  mbaya  zaidi  tunaweza  kupata  masoko  katika  nchi  za Kenya ,  Uganda , Msumbiji , Burundi  na  Jamhuri  ya  kidemokrasia  ya  congo “
Alisema  kuwa   kiwanda  kimeweza  kutoa  ajira  kwa  vijana  150  kati ya  hao  ajira  ya  kudumu  ni  watu  105  na  ajira ya  muda  n  watu  45 .
Pia  alisema   kiwanda   hicho  kimeweza kuzaa kiwanda  kingine   cha pipi  ambapo ujenzi   umekamilika  na  mashine   zimeshafika  ndani ya  kipindi  cha miezi mitatu  hadi  mine  kitaanza kazi  ya uzalishaji  na  kutoa ajira kwa  vijana 60.
Bwana  Thakore alizitaja  changamoto  zinazokabili  kiwanda  hicho  kuwa  ni sukari  ya  viwandani ambayo  waliomba tani 3000  kwa mwaka huu  wa serikali 2017/18  ila  wamepata  tani 416  mwezi  Oktoba .
  Jumla ya  mzigo  wote  ambao  tumepata  ni tani 848 ambao  tumepokea  lakini baada ta  timu  ya  Vwrification  kupita  kwetu  na  tarehe  19  Januari  mwaka  huu  hadi  sasa  hakuna  majibu  yoyote  juu ya  vibali  vingine  kwa bodi ya  sukari  wamekataa  kutoa  vibali   vingine  hadi pale  ambapo  maelekezo  yatatolewa   hivyo  basi  tunakosa  mwelekeo  wa  huko mbele  kwa kuwa malighafi  hiyo  muhimu    ikiadimika  tutalazimika  kusimama  uzalishaji “
Alisema  wanaomba serikali  kusikia  kilio  chao  kwa  kutafuta  ufumbuzi wa  haraka wa  jambo hilo zito .

“ Ili   serikali  itusaidie   kuhakikisha  bodi ya  sukari  iweze   kutupa  muongozo  wa  juu ya  vibali  vingine  kabla  hatujaagiza mzigo mwingine  na  kabla ya akiba  tuliyo nayo  kuisha  kwa maana  mzigo  hadi ufike kiwandani   unachukua  muda wa miezi miwili  jambo  hili  ni muhimu  sana  katika maendeleo ya  viwanda  vyetu  na kwa  kuwa  tunaongeza mitambo  ya pipi   tunahitaji  Sukari kwa  wingi  kutokana na kuongezeka  uzalishaji “

Alisema  baada ya  serikali ya a wamu ya  tano chini ya Rais Dkt  John  Magufuli   kuingia madakani  soko la ndani  limeongezeka   kutokana na  serikali   kubana njia  za  kukwepa  ushuru  wa bandarini .

  Kubanwa  kwa  mianya ya  ukwepaji kodi  kumesaidia   sana  kuongeza  soko la  bidhaa  zetu  awali  bidhaa  kutoka  nje  zilikuwa zikiuzwa kwa  bei  ndogo hasa  baada ya  ukwepaji  wa kodi   na  kuhatarisha  bidhaa  za ndani .

 
Copyright © 2014 Mkono Wangu Production Designed by EvMak Tanzania